باب استحباب وصية أهل المريض ومن يخدمه بالإحسان إليه والصبر عَلَى مَا يشق من أمره وكذا الوصية بمن قرب سبب موته بحد أَوْ قصاص ونحوهما
عن عِمران بن الحُصَين رضي اللَّه عنهما أَن امرأَةً مِنْ جُهَيْنَةَ أَتَتِ النبيَّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم وهِي حُبْلَى مِنَ الزِّنَا، فَقَالَتْ: يَا رسول اللَّهِ، أَصبتُ حَدّاً فَأَقمْهُ علَيَّ، فَدعا رسولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم وليَّهَا، فقالَ: “أَحْسِنْ إِلَيْهَا، فَإِذا وضَعتْ فَأْتِني بِهَا”فَفعلَ فَأَمر بِها النبيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فشُدَّتْ علَيها ثِيابُها، ثُمَّ أَمر بِها فَرُجِمتْ، ثُمَّ صَلَّى عَلَيْهَا. رواه مسلمٌ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
148. MLANGO WA SUNNAH YA KUWAUSIA FAMILIA YA MGONJWA NA ANAYEMHUDUMIKIA KUMTENDEA WEMA, KUMCHUKULIA NA KUMSUBIRIA JUU YA LINALOWATIA MASHAKA KWA SABABU YA MARADHI YAKE, VILEVILE KUMWUSIA AMBAYE SABABU YA MAUTI IMEMFIKIA KWA SABABU YA HADDI (ADHABU), AU KISASI NA MFANO WAKE
Imepokewwa na ‘Imrân bin al-Husain (Radhi za Allah ziwe juu yao) amesimulia kuwa, mwanamke kutoka kabila la Juhainah alimwendea Mtume ﷺ naye ana mimba ya zinaa, akamwambia: “Yâ Rasûlallâh, nimetenda dhambi inayopasisha haddi, kwa hivyo nipitishie.” Mtume ﷺ akamwita msimamizi wake, akamwambia: “Mfanyie hisani, atakapojifungua mlete.” Yule msimamizi akafanya kama alivyoamrishwa, halafu akaja naye. Mtume ﷺ akaamuru, akafungwa kwa nguo zake, halafu akaamuru akarajimiwa, halafu akamswalia.” [ Imepokewa na Muslim ]