0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

Sahih Al-Bukhari Kitabu cha Imani Mlango Wa neno lake Mtume isemayo: “Uislamu umejengwa juu ya Nguzo tano”


صحيح البخاري


كِتَابُ الإِيمَانِ

«بَابُ قَوْلِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «بُنِيَ الإِسْلاَمُ عَلَى خَمْسٍ

وَهُوَ قَوْلٌ وَفِعْلٌ، وَيَزِيدُ وَيَنْقُصُ، قَالَ اللَّهُ تَعَالَى {لِيَزْدَادُوا إِيمَانًا مَعَ إِيمَانِهِمْ} [الفتح: 4] {وَزِدْنَاهُمْ هُدًى} [الكهف: 13] {وَيَزِيدُ اللَّهُ الَّذِينَ اهْتَدَوْا هُدًى} [مريم: 76] {وَالَّذِينَ اهْتَدَوْا زَادَهُمْ هُدًى وَآتَاهُمْ تَقْوَاهُمْ} [محمد: 17] وَقَوْلُهُ: {وَيَزْدَادَ الَّذِينَ آمَنُوا إِيمَانًا} [المدثر: 31] وَقَوْلُهُ: {أَيُّكُمْ زَادَتْهُ هَذِهِ إِيمَانًا فَأَمَّا  الَّذِينَ آمَنُوا فَزَادَتْهُمْ إِيمَانًا} [التوبة: 124] وَقَوْلُهُ جَلَّ ذِكْرُهُ: {فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَانًا} [آل عمران: 173] وَقَوْلُهُ تَعَالَى: {وَمَا زَادَهُمْ إِلَّا إِيمَانًا وَتَسْلِيمًا} [الأحزاب: 22] وَالحُبُّ فِي اللَّهِ وَالبُغْضُ فِي اللَّهِ مِنَ الإِيمَانِ ” وَكَتَبَ عُمَرُ بْنُ عَبْدِ العَزِيزِ إِلَى عَدِيِّ بْنِ عَدِيٍّ: «إِنَّ لِلْإِيمَانِ فَرَائِضَ، وَشَرَائِعَ، وَحُدُودًا، وَسُنَنًا، فَمَنِ اسْتَكْمَلَهَا اسْتَكْمَلَ الإِيمَانَ، وَمَنْ لَمْ يَسْتَكْمِلْهَا لَمْ يَسْتَكْمِلِ الإِيمَانَ، فَإِنْ أَعِشْ فَسَأُبَيِّنُهَا لَكُمْ حَتَّى تَعْمَلُوا بِهَا، وَإِنْ أَمُتْ فَمَا أَنَا عَلَى صُحْبَتِكُمْ بِحَرِيصٍ» وَقَالَ إِبْرَاهِيمُ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «وَلَكِنْ لِيَطْمَئِنَّ قَلْبِي» وَقَالَ مُعَاذُ بْنُ جَبَلٍ: «اجْلِسْ بِنَا نُؤْمِنْ سَاعَةً» وَقَالَ ابْنُ مَسْعُودٍ: «اليَقِينُ الإِيمَانُ كُلُّهُ» وَقَالَ ابْنُ عُمَرَ: «لاَ يَبْلُغُ العَبْدُ حَقِيقَةَ التَّقْوَى حَتَّى يَدَعَ مَا حَاكَ فِي الصَّدْرِ» وَقَالَ مُجَاهِدٌ: «شَرَعَ لَكُمْ مِنَ الدِّينِ أَوْصَيْنَاكَ يَا مُحَمَّدُ وَإِيَّاهُ دِينًا وَاحِدًا» وَقَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ: «شِرْعَةً وَمِنْهَاجًا» سَبِيلًا وَسُنَّةً


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ مُحَمّد بن صَالِح العُثَيْمِين رحمه الله تعالى



Sahih Al-Bukhari


MLANGO WA NENO LAKE MTUME ISIMAYO : “UISLAMU UMEJENGWA JUU YA NGUZO TANO

Nayo (Imani) ni kauli na kitendo, huzidi na hupungua. Allâh Amesema: “… ili wazidi Imani juu ya Imani yao.” [48: 4]. “Na Sisi tukawazidisha uwongofu. [18: 13]. Na Allâh Huwazidishia uwongofu wenye kushika uwongofu.” [19: 76]. Na wale walioongoka Anawazidishia uongofu na Anawapa uchamngu wao.” [47: 17]. na wazidi Imani wale walio amini. [74: 31]. “Ni nani miongoni mwenu (Sura) hii imemzidishia Imani? Ama wale walioamini, imewazidishia Imani.” [9: 124]. “Waogopeni! Hayo yakawazidishia Imani.” [3: 173]. “Na hayo hayakuwazidisha ila Imani na utiifu.” [33: 22]. Kupenda kwa ajili ya Allâh na kuchukia kwa ajili ya Allâh ni katika Imani.

Umar bin Abdil-Azîz alimwandikia Adiyyi bin Adiyyi: Imani ina faradhi, Sharia, mipaka na sunna (mienendo), anayeikamilisha atakuwa ameshakamilisha Imani, na ambaye hakuikamilisha, atakuwa bado hajakamilisha Imani. Nitakapoishi, nitawabainishia ili muifanyie amali, na iwapo nitakufa, mimi sina pupa ya kusuhubiana nanyi. Ibrâhîm ﷺ alisema: “Ili yakini yangu ipate kuzidi.” Mu‘âdh bin Jabal alimwambia mtu: “Keti nasi tuamini muda mchache.”Abdullâh bin Mas‘ûd amesema: “Yakini ndio Imani yote.” ‘Abdullâh bin ‘Umar amesema: “Mja hawezi kuifikia hakika ya Taqwa (uchamungu) mpaka aliache linalomtia shaka moyoni. Asema Mujâhid (katika kuifafanua Aya hii:) Amewaamrisha Dini [42: 13] kwa kusema: Tumekuusia wewe ewe Muhammad na yeye (Nuhu) muwe na Dini moja. Abdullâh bin Abbâs ameifafanua Aya hii: Sharia yake na njia yake.” [5: 48] kwa kusema: Njia na mwenendo.


Begin typing your search above and press return to search.