باب بيان أنَّ السنة إِذَا قيل للمستأذن: من أنت؟ أن يقول: فلان فيسمي نفسه بما يعرف به من اسم أَوْ كنية وكراهة قوله”أنا”ونحوها
عن أنس رضي الله عنه في حديثه المشهور في الإسراءِ قَالَ: قَالَ رسول الله صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم، “ثُمَّ صَعِدَ بي جِبْريلُ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنيا فَاسْتَفْتَحَ”فقِيلَ: منْ هذَا؟ قَالَ: جبْريلُ، قِيلَ: وَمَنْ مَعَك؟ قَالَ: مُحمَّدٌ. ثمَّ صَعِدَ إلى السَّماء الثّانية وَالثَّالِثَةِ والرَّابعة وَسَائرهنَّ وَيُقالُ فِي بَابِ كُلِّ سَمَاءٍ: مَنْ هَذَا؟ فَيقُولُ: جِبْريلُ” متفقٌ عَلَيْهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
141. MLANGO WA KUBAINISHA KUWA SUNNAH NI MTU ANAPOULIZWA: “NI NANI WEWE?” AJIBU: “NI FULANI,” AJITAJE KWA JINA ANALOJULIKANA KWALO AU KWA LAKABU, NA MAKRUHU YA KUJIBU: “NI MIMI,” NA MFANO WAKE
Imepokewa na Anas (Radhi za Allah ziwe juu yake) ameeleza katika ile Hadîth yake mashuhuri ya Isrâ: “Mtume ﷺ akasema: “Kisha Jibrîl akapanda nami hadi katika wingu wa dunia, akabisha ili afunguliwe, akaulizwa: “Ni nani huyu?” Akajibu: “Ni Jibrîl,” akaulizwa: “Ni nani aliye pamoja nawe?” Akajibu: “Ni Muhammad.” Kisha akapanda katika wingu wa pili, akabisha ili afunguliwe, akaulizwa: “Ni nani huyu?” Akajibu: “Ni Jibrîl,” akaulizwa: “Ni nani aliye pamoja nawe?” Akajibu: “Ni Muhammad,” akapanda wingu wa tatu, wingu wa nne na mbingu nyenginezo, na akiulizwa katika mlango wa kila wingu: “Ni nani huyu?” Naye akijibu: “Ni Jibrîl.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim].