باب سلام الرجل على زوجته والمرأة من محارمه وعلى أجنبية وأجنبيات لا يخاف الفتنة بهن وسلامهن بهذا الشرط
عن سهل بن سعدٍ رضي الله عنه قال: كانَتْ فِينَا امْرَأَةٌ وفي رواية: – كانَتْ لَنا عَجُوزٌ تأْخُذُ منْ أَُصُولِ السِّلْقَ فتطْرَحُهُ فِي القِدْرِ وَتُكَرْكِرُ حَبَّاتٍ منْ شَعِيرٍ، فَإذَا صَلَّيْنا الجُمُعَةَ وانْصَرَفْنَا نُسَلِّمُ عَلَيْها فَتُقدِّمُهُ إليْنَا رواه البخاري
قَوْله”تُكَرْكِرُ”أي تَطحَنُ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
137. MLANGO WA MTU KUMTOLEA SALAMU MKEWE NA MWANAMKE AMBAYE NI MAHARIMU YAKE, NA AMBAYE NI AJINABI ASIPOCHELEA FITNA YAO NA WAO (WANAWAKE) KUTOA SALAMU KWA SHARTI KAMA HII
Imepokewa na Sahl bin Sa’d (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Kulikuwa kuna mwanamke miongoni mwetu – katika riwaya nyingine imesema: “Kulikuwa kuna ajuza – akichukua mizizi ya kiazisukari (cheupe) akitia sufuriani na akisaga nafaka za shayiri. Tunapomaliza kuswali Swala ya Ijumaa na tukaenda zetu, tukimtolea salamu naye akituletea.” [ Imepokewa na Bukhari.]