0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

130 KUOMBA MASAMAHA NA KUTUBIA

KINGA YA MUISLAMU

[ قال رسول الله صلى الله عيه وسلم :[ والله إني لاستغفر الله وأتوب إليه في اليوم أكثر من سبعين مرة

 البخاري مع الفتح 11/101

Amesema Mtume ﷺ [Naapa kwa Mwenyezi Mungu  hakika mimi ninamtaka msamaha Mwenyezi Mungu  na ninatubia kwake katika kila siku zaidi ya mara sabini.]      [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

[ وقال صلى الله عيه وسلم :[ يا أيها الناس توبوا إلى الله فإني أتوب في اليوم إليه مائة مرةً

مسلم 4/2076

Mtume ﷺ amesema: [Enyi watu tubieni kwa Mwenyezi Mungu  kwani mimi ninatubia kwake kwa siku mara mia.]       [Imepokewa Muslim.]

[وقال صلى الله عيه وسلم :[ من قال أستغفر الله العظيم الذي لا إله إلا هو الحي القيوم وأتوب إليه ، غفر الله لهُ وإن كان فر من الزحف

أخرجه أبو داود 2/85 والترمذي 5/569 والحاكم وصححه ووافقه الذهبي

Amesema Mtume ﷺ  yoyote anaesema :

[Namuomba msamaha Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila Yeye, aliye Hai aliyesimama kwa dhati yake, na ninarejea kwake.]       Mwenyezi Mungu atamsamehe hata kama ana makosa ya kukimbia vitani.     [Imepokewa na abuu Daud na  Al-Ttirmidhiy na Al-Haakim.]

 

[ وقال صلى الله عيه وسلم :[ أقرب ما يكون الربُّ من العبد في جوف الليل الآخر فإن استطعت أن تكون ممن يذكر الله في تلك الساعة فكن

أخرجه الترمذي والنسائي 1/279 والحاكم

Na Amesema Mtume ﷺ [Wakati anaokuwa mja na Mola wake wako karibu zaidi ni katika nusu ya mwisho wa usiku.  Ukiweza kuwa miongoni mwa wanaomtaja  Mwenyezi Mungu  kwa wakati huo basi kuwa]         [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy na Al-Nnasaai na Al-Haakim.]

[وقال صلى الله عيه وسلم :[ أقرب ما يكون العبد من ربه وهو ساجد فأكثروا الدعاء

مسلم 1/350

Na Mtume ﷺ amesema:  [Sehemu ambayo anakuwa mja yuko karibu mno na Mola wake ni wakati amesujudu, basi zidisheni dua wakati huo.]      [Imepokewa na Muslim.]

[وقال صلى الله عيه وسلم :[ إنه ليغان على قلبي وإني لاستغفرُ الله في اليوم مائة مرة

 أخرجه مسلم 4/2075

Na Mtume ﷺ amesema: [Huwa nimesahaulishwa kumtaja Mwenyezi Mungu  na hakika mimi ninamuomba msamaha Mwenyezi Mungu  mara mia kwa siku.]     [Imepokewa na Muslim.]

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.