0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

120. Riyadhu Swalihina Mlango wa Ubainifu wa Njia nyingi za Kheri Hadithi ya 04


BUSTANI YA WATU WEMA


1463655589


عن أَبِي ذرٍّ رضي اللَّه عنه : أنَّ ناساً قالوا : يا رسُولَ اللَّهِ ، ذَهَب أهْلُ الدُّثُور بالأجُورِ ، يُصَلُّونَ كَمَا نُصَلِّى ، وَيَصُومُونَ كَمَا نَصُومُ ، وَيَتَصَدَّقُونَ بَفُضُولِ أمْوَالهِمْ قال : «أوَ لَيْس قَدْ جَعَلَ لَكُمْ مَا تَصَدَّقُونَ بِهِ : إنَّ بِكُلِّ تَسْبِيحَةٍ صَدقَةً، وكُلِّ تَكبِيرةٍ صدقة ، وكلِّ تَحْمِيدةٍ صدقةً ، وكلِّ تِهْلِيلَةٍ صَدقَةً ، وأمرٌ بالمعْرُوفِ صدقةٌ ، ونَهْىٌ عنِ المُنْكر صدقةٌ وفي بُضْعِ أحدِكُمْ صدقةٌ » قالوا : يا رسولَ اللَّهِ أيأتي أحدُنَا شَهْوَتَه ، ويكُونُ لَه فيها أجْر ؟، قال : «أرأيْتُمْ لو وضَعهَا في حرامٍ أَكَانَ عليهِ وِزْرٌ ؟ فكذلكَ إذا وضَعهَا في الحلاَلِ كانَ لَهُ أجْرٌ»   رواه مسلم


Kutoka Abuu Dharr, Jundub bin Junaadah Radhi za Allah ziwe juu kwamba Baadhi ya watu (walimuendea Mtume ﷺ) wakamwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu , matajiri wamechukua thawabu zote. Wao wanaswali kama tunavyoswali, na wanafunga kama tunavyofunga na wanatoa sadaka katika mali yao iliyobaki. (Mtume ﷺ) Akawaambia: [Nanyi pia Mwenyezi Mungu Amewajaalia cha kutolea sadaka; kila Tasbihi  (Kusema Subhaana Allaah) ni sadaka, na kila Takbiri (Kusema Allaahu Akbar) ni sadaka, na kila Tahliil (Kusema Laa ilaaha illa-Allaah) ni sadaka, na kila Tahmid (Kusema AlhamduliLLaah) ni sadaka. na Kuamrisha mema ni sadaka na kukataza maovu ni sadaka, na mmoja wenu anapo muingilia mkewe ni sadaka.] Wakauliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mmoja wetu anaenda kufanya matamanio yake na awe amepata Thawabu? Akawaambia: [Mwaonaje lau kitendo kile atakifanya kwa njia ya haraam, si atapata dhambi? Vile vile atakapokitenda kwa njia ya halaal atakuwa na ujira.]    [Imepokewa na Muslim]


 شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.