0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

1175. Riyadhu Swalihina Mlango wa fadila ya kuswali Usiku


٢١٢- باب فضل قيام الليل


وعَنْ حُذيفَهَ رَضِيَ اللَّه عنْهُ، قَالَ: صَلَّيْتُ مَعَ النَّبِيَّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم، ذاتَ لَيْلَةٍ فَافْتَتَح البقَرَةَ، فقلتُ: يَرْكَعُ عِنْدَ المِئَةِ، ثُمَّ مَضَى، فقلتُ: يُصَلَّي بِهَا في ركْعَةٍ، فمَضَى، فَقُلْتُ: يَرْكَعُ بِهَا، ثُمَّ افْتَتَح النِّسَاءَ فَقَرأَهَا، ثُمَّ افْتَتَحَ آلَ عِمْرَانَ، فَقَرَأَها، يَقْرَأُ مُتَرَسِّلاً إِذا مَرَّ بِآيَةِ فِيها تَسْبيحٌ سَبَّحَ، وَإِذا مَرَّ بِسُؤَالٍ سَأَلَ، وَإذَا مَرَّ بتَعوَّذ تَعَوَّذَ، ثُمَّ رَكَعَ، فجعَل يَقُولُ:” سُبْحَانَ ربِّي العظيمِ ” فَكَانَ رُكُوعُهُ نَحْواً مِنْ قِيَامِهِ، ثُمَّ قَالَ: “سمِع اللَّه لمَنْ حَمِدَه، رَبَّنَا لَكَ الحْمدُ” ثُمَّ قامَ طَويلاً قَرِيباً مِمَّا رَكَعَ، ثُمَّ سَجد فَقَالَ: “سُبْحانَ رَبِّيَ الأَعْلى ” فَكَانَ سَجُودُهُ قَرِيباً مِنْ قِيَامِهِ.     رواه مسلم


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



213. MLANGO WA FADHILA YA KUSWALI USIKU


Imepokewa kutaka kwa Hudhaifa ( Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Usiku mmoja Niliswali pamoja na Mtume , akaanza kusoma Sûratul-Baqarah. Nikasema (moyoni), atarukuu katika Aya ya mia, akaendelea, nikasema ataimaliza Sura yote katika rakaa moja, akaendelea, nikasema atarukuu akiimaliza Sura hii, halafu akaianza Sûratunnisâ, akaisoma, kisha akaianza Sûratu Âli ‘Imrân, akaisoma yote; alikuwa akisoma taratibu, anapoisoma Aya yenye kumsabihi Allâh, yeye humsabihi, anapoisoma Aya ya kuomba, yeye huomba na anapoisoma Aya ya kujilinda yeye hujilinda, kisha akarukuu, akawa anasema: “Subhâna rabbiyal ‘adhwîm,” kurukuu kwake kukawa kunafanana na kisimamo chake, kisha akasema: “Sami‘allâhu liman hamidah rabbanâ lakalhamd,” kisha akasimama kisimamo kirefu kinachokaribiana na rukuu, kisha akasujudu, akasema: “Subhâna rabbiyal-a’lâ,” kusujudu kwake kukakaribiana na kisimamo chake.”    [ Imepokewa na Muslim ].


Begin typing your search above and press return to search.