٢١٢- باب فضل قيام الليل
وعَنْ عائِشة رضي اللَّه عنْهَا، أَنَّ رَسولَ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم كَان يُصلِّي إِحْدَى عَشرَةَ رَكْعَةً تَعْني في اللَّيْلِ يَسْجُدُ السَّجْدَةَ مِنْ ذلكَ قَدْر مَا يقْرَأُ أَحدُكُمْ خَمْسِين آيَةً قَبْلَ أَن يرْفَعَ رَأْسهُ، ويَرْكَعُ رَكْعَتَيْنِ قَبْل صَلاةِ الفَجْرِ، ثُمَّ يضْطَجِعُ عَلَى شِقِّهِ الأَيمْنِ حَتَّى يأْتِيَهُ المُنَادِي للصلاةِ، رواه البخاري
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
213. MLANGO WA FADHILA YA KUSWALI USIKU
Imepokewa kutaka kwa ‘Âisha ( Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Mtume ﷺ alikuwa akiswali rakaa kumi na moja – yaani usiku – akisujudu kiasi cha mmoja wenu anavyosoma Aya hamsini kabla ya kuinua kichwa chake, na akiswali rakaa mbili kabla ya Swala ya alfajiri, kisha akiegemea kwa ubavu wake wa kulia mpaka aendewe na muadhini wa Swala.” [ Imepokewa Bukhârî ].