٢١٢- باب فضل قيام الليل
وعن أَبي هُريرَةَ، رَضِي اللَّه عَنْهُ، أَنَّ رسُولَ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قالَ: “يَعْقِدُ الشَّيْطَانُ عَلى قافِيةِ رَأْسِ أَحَدِكُم، إِذا هُوَ نَامَ، ثَلاثَ عُقدٍ، يَضرِب عَلى كلِّ عُقدَةٍ: عَلَيْكَ ليْلٌ طَويلٌ فَارقُدْ، فإِنْ اسْتَيْقظَ، فَذَكَرَ اللَّه تَعَالَى انحلَّت عُقْدَةٌ، فإِنْ توضَّأَ انحَلَّت عُقدَةٌ، فَإِن صلَّى انحَلَّت عُقدُهُ كُلُّهَا، فأَصبَحَ نشِيطاً طَيِّب النَّفسِ، وَإِلاَّ أَصبح خَبِيثَ النَّفْسِ كَسْلانَ” متفقٌ عَلَيْهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
213. MLANGO WA FADHILA YA KUSWALI USIKU
Imepokewa kutaka kwa Abû Huraira ( Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia kuwa Mtume ﷺ amesema: “Shetani hupiga fundo katika kishogo cha mmoja wenu wakati anapolala, hupiga mafundo matatu, akimwambia katika kila fundo: unayo nafasi ya usiku mrefu, lala. Atakapoamka na akamtaja Allâh Mtukufu, kifundo (cha kwanza) hufunguka, akitawadha, kifundo kingine hufunguka na akiswali, kifundo kingine hufunguka, akapambaukiwa mchangamfu na mwenye furaha moyoni. Asipofanya hivyo, hupambaukiwa ilihali ni mzito wa nafsi na ni mvivu.” [ Wameaikiana bukhari na Muslim ].