٢١٠- باب فضل يوم الجمعَة ووُجوبها والاغتِسال لَهَا والتطيّب والتبكير إِلَيْهَا والدعاء يوم الجمعة والصلاة عَلَى النبيّ صلى الله عليه وسلم فيه وبيان ساعة الإجابة واستحباب إكثار ذكر الله بعد الجمعة
وَعنْ أَبي بُردةَ بنِ أَبي مُوسى الأَشعَرِيِّ رَضِيَ اللَّه عَنْهُ، قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ ابنُ عُمرَ رضَيَ اللَّه عنْهُمَا: أَسَمِعْت أَبَاكَ يُحَدِّثُ عَن رَسُول اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم في شَأْنِ ساعَةِ الجُمُعَةِ؟ قَالَ: قلتُ: نعمْ، سَمِعتُهُ يقُولُ: سمِعْتُ رسُولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يَقُولُ: ” هِيَ مَا بيْنَ أَنْ يَجلِسَ الإِمامُ إِلى أَنْ تُقضَى الصَّلاةُ ” رواه مسلم
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
210. MLANGO WA FADHILA YA SIKU YA IJUMAA, KUPASA KWAKE, KUOGA KWA AJILI YA SWALA HIYO, KUJIPAKA MANUKATO, KUENDA MAPEMA, KUOMBA DUA SIKU YA IJUMAA, KUMSWALIA MTUME ﷺ KATIKA SIKU HIYO, KUBAINISHA SAA YA KUJIBIWA DUA NA SUNNAH YA KUKITHIRISHA KUMTAJA ALLÂH BAADA YA SWALA YA IJUMAA
Imepokewa kutaka kwa Abû Burdah bin Abû Mûsâ al-Ash‘ary ( Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: ‘Abdullâh bin ‘Umar ( Radhi za Allah ziwe juu yao) aliniuliza: “Uliwahi kumsikia baba yako akikuhadithia kutoka kwa Mtume ﷺ kuhusu saa ya Ijumaa?” Nikamjibu: “Ndio, nilimsikia akisema: “Nimemsikia Mtume ﷺ akisema: “(Saa hiyo) ni baina ya imamu kuketi (juu ya mimbari) mpaka Swala imalizike kuswaliwa.” [ Imepokewa na Muslim.]