٢١٠- باب فضل يوم الجمعَة ووُجوبها والاغتِسال لَهَا والتطيّب والتبكير إِلَيْهَا والدعاء يوم الجمعة والصلاة عَلَى النبيّ صلى الله عليه وسلم فيه وبيان ساعة الإجابة واستحباب إكثار ذكر الله بعد الجمعة
وعَنْ أَبي هُريرةَ رضي اللَّه عَنْهُ، أَنَّ رَسُولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قَالَ: ” مَن اغْتَسَلَ يَوْم الجُمُعَةِ غُسْلَ الجنَابَةِ، ثُمَّ رَاحَ في الساعة الأولى، فكَأَنَّمَا قرَّبَ بَدنَةً، ومنْ رَاحَ في السَّاعَةِ الثَّانِيَة، فَكأنَّما قَرَّبَ بَقَرَةً، وَمَنْ رَاحَ في السَاعَةِ الثَالِثةِ، فَكأنَّما قَرَّبَ كَبْشاً أَقرَنَ، ومنْ رَاحَ في السَّاعَةِ الرَّابِعةِ، فَكأنَّما قَرَّبَ دَجَاجَةً، ومنْ رَاحَ في السَّاعَةِ الخامِسةِ فَكأنَّما قَرَّبَ بيْضَةً، فَإِذا خَرَج الإِمامُ، حَضَرَتِ الملائِكَةُ يَسْتمِعُونَ الذِّكرَ “ متفقٌ عَلَيْهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
210. MLANGO WA FADHILA YA SIKU YA IJUMAA, KUPASA KWAKE, KUOGA KWA AJILI YA SWALA HIYO, KUJIPAKA MANUKATO, KUENDA MAPEMA, KUOMBA DUA SIKU YA IJUMAA, KUMSWALIA MTUME ﷺ KATIKA SIKU HIYO, KUBAINISHA SAA YA KUJIBIWA DUA NA SUNNAH YA KUKITHIRISHA KUMTAJA ALLÂH BAADA YA SWALA YA IJUMAA
Imepokewa kutaka kwa Abû Huraira ( Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia kuwa Mtume ﷺ amesema: “Atakayeoga siku ya Ijumaa kama anavyooga janaba, kisha akaenda (Msikitini) saa ya kwanza, atakuwa ni kama alietoa sadaka ya ngamia. Atakayeenda katika saa ya pili, atakuwa ni kama alietoa sadaka ya ng’ombe. Atakayeenda katika saa ya tatu, atakuwa ni kama alietoa sadaka ya kondoo mwenye pembe. Atakayeenda katika saa ya nne, atakuwa ni kama alietoa sadaka ya kuku. Atakayeenda katika saa ya tano, atakuwa ni kama alietoa sadaka ya yai. Imamu atakapopanda juu ya mimbari, Malaika wanahudhuria wakisikiliza mawaidha.” [ Wameafikiana Bukhârî na Muslim.]