٢١٠- باب فضل يوم الجمعَة ووُجوبها والاغتِسال لَهَا والتطيّب والتبكير إِلَيْهَا والدعاء يوم الجمعة والصلاة عَلَى النبيّ صلى الله عليه وسلم فيه وبيان ساعة الإجابة واستحباب إكثار ذكر الله بعد الجمعة
وعَنْ أَبي هُريرةَ رَضِيَ اللَّه وَعَنْهُ وعَنِ ابنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّه عَنْهُمْ، أَنَّهما سَمِعَا رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقولُ عَلَى أَعْوَادِ مِنْبَرِهِ: “لَيَنْتَهِيَنَّ أَقْوَامٌ عَنْ وَدْعِهِمُ الجمُعَاتِ، أَوْ لَيَخْتِمَنَّ اللَّه عَلَى قُلُوبِهمْ، ثُمَّ ليَكُونُنَّ مِنَ الغَافِلينَ” رواه مسلم.
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
210. MLANGO WA FADHILA YA SIKU YA IJUMAA, KUPASA KWAKE, KUOGA KWA AJILI YA SWALA HIYO, KUJIPAKA MANUKATO, KUENDA MAPEMA, KUOMBA DUA SIKU YA IJUMAA, KUMSWALIA MTUME ﷺ KATIKA SIKU HIYO, KUBAINISHA SAA YA KUJIBIWA DUA NA SUNNAH YA KUKITHIRISHA KUMTAJA ALLÂH BAADA YA SWALA YA IJUMAA
Imepokewa kutaka kwa Abû Huraira na ‘Abdullâh bin ‘Umar ( Radhi za Allah ziwe juu yao) wamesimulia kuwa wamemsikia Mtume ﷺ akisema naye yuko juu ya mimbari yake: “Hakika watu watakoma kuacha Swala za Ijumaa, au Allâh Atapiga muhuri juu ya nyoyo zao, kisha watakuwa miongoni mwa walioghafilika!” [ Imepokewa na Muslim.]