0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

1131. Riyadhu Swalihina Mlango wa Sunna ya kuswali Nafla nyumbani ima iwe ni ya Ratiba au nyongeza, na Maamrisho ya kugeuka katika Sunna pahali pa faradhi….


٢٠٤- باب استحباب جعل النوافل في البيت سواء الراتبة وغيرُها والأمر بالتحول للنافلة من موضع الفريضة أَو الفصل بينهما بكلام


وَعنْ عُمَر بْنِ عطاءٍ أَنَّ نَافِعَ بْنَ حُبَيْر أَرْسلَهُ إِلَى السَّائِب ابن أُخْتِ نَمِرٍ يَسْأَلُهُ عَنْ شَيْءٍ رَآهُ مِنْهُ مُعَاوِيةُ في الصَّلاةِ فَقَالَ: نَعمْ صَلَّيْتُ مَعَهُ الجُمُعَةَ في المقصُورَةِ، فَلَمَّا سَلَّمَ الإِمامُ، قُمتُ في مقَامِي، فَصلَّيْتُ، فَلَما دَخل أَرْسلَ إِليَّ فَقَالَ: لاَ تَعُدْ لِمَا فعَلتَ: إِذَا صلَّيْتَ الجُمُعةَ، فَلا تَصِلْها بصلاةٍ حَتى تَتَكَلَّمَ أَوْ تخْرُجَ، فَإنَّ رسولَ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم أَمرَنا بِذلكَ، أَنْ لاَ نُوصِلَ صَلاَةً بصلاةٍ حتَّى نَتَكَلَّمَ أَوْ نَخْرُجَ.     رواه مسلم


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



204. MLANGO WA SUNNAH YA KUSWALI NAFLA NYUMBANI, IMA IWE NI YA RATIBA AU NYENGINEZO, NA MAAMRISHO YA KUGEUKA KATIKA SUNNAH MAHALA PA FARADHI AU KUPAMBANUA KWA MANENO BAINA YAKE


Imepokewa kutoka kwa ‘Umar bin ‘Atâ amesimulia kuwa Nâfi’ bin Jubair alimtuma kwa as-Sâ-ib ambaye ni mpwa wa Namir amwulize jambo aliloonekaniwa na Mu‘âwiya akilitenda katika Swala na akamwambia: “Niliswali pamoja naye Swala ya Ijumaa katika chumba (cha Msikiti), imamu alipotoa salamu nilisimama mahala pangu nikaswali. Alipoingia, alinitumia mtu akaniambia: “Usirudie kitendo ulichokifanya; unapomaliza kuswali Swala ya Ijumaa, usiunge Swala yoyote mpaka uzungumze au utoke (Msikitini), kwani Mtume alituamrisha kufanya hivyo; tusiunge Swala yoyote kwa Swala nyingine mpaka tuzungumze au tutoke.”      [ Imepokewa na Muslim ].


Begin typing your search above and press return to search.