٢٠٤- باب استحباب جعل النوافل في البيت سواء الراتبة وغيرُها والأمر بالتحول للنافلة من موضع الفريضة أَو الفصل بينهما بكلام
وعَنْ جابرٍ رَضِي اللَّه عَنْهُ قالَ: قَالَ رسولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: “إِذَا قَضَى أَحَدُكُمْ صلاتَهُ في مسْجِدِهِ، فَلَيجْعَلْ لِبَيْتهِ نَصِيباً مِنْ صَلاتِهِ، فَإنَّ اللَّه جَاعِلٌ في بيْتِهِ مِنْ صلاتِهِ خَيْراً” رواه مسلم
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
204. MLANGO WA SUNNAH YA KUSWALI NAFLA NYUMBANI, IMA IWE NI YA RATIBA AU NYENGINEZO, NA MAAMRISHO YA KUGEUKA KATIKA SUNNAH MAHALA PA FARADHI AU KUPAMBANUA KWA MANENO BAINA YAKE
Imepokewa kutoka kwa Jâbir (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Mtume ﷺ amesema: “Mmoja wenu anapomaliza kuswali Msikitini mwake, basi ajaalie nyumbani mwake kuwa na fungu la Swala yake; hakika Allâh Hujaalia kheri katika nyumba yake kutokana na kuswali kwake.” [ Imepokewa na Muslim ].