٢٠١- باب سُنَّة المغرب بَعدَها وقبلَها
وعن أَنسٍ رَضيَ اللَّه وعَنْهُ قَالَ: كُنَّا نُصَلِّي عَلى عَهدِ رسولِ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم رَكعَتيْنِ بعدَ غُروبِ الشَّمْس قَبلَ المَغربِ، فقيلَ: أَكانَ رسولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم صَلاَّهُمَا؟ قَالَ: كانَ يَرانَا نُصَلِّيهِمَا فَلَمْ يَأْمُرْنَا وَلَمْ يَنْهَنا. رَوَاه مُسْلِمٌ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
201. MLANGO WA SUNNAH YA MAGHARIBI BAADA YAKE NA KABLA YAKE
Imepokelewa kutoka kwa Anas (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: ““Tulikuwa – zama za Mtume ﷺ – tukiswali rakaa mbili baada ya jua kuzama kabla ya magharibi.” Akaulizwa: “Je, Mtume ﷺ alikuwa akiziswali?” Akajibu: “Alikuwa akituona tukiziswali, na hakutuamrisha wala hakutukataza.” [ Imepokewa na Muslim. ]