١٩٦- باب تأكيد ركعتي سنَّةِ الصبح
وعنْ أَبي عبدِ اللَّهِ بِلالِ بنِ رَبَاحٍ رضيَ اللَّه عنْهُ، مُؤَذِّنِ رسولِ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم أَنَّهُ أَتَى رَسُولَ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم لِيُؤذِنَه بِصَلاةِ الغدَاةِ، فَشَغَلتْ عَائشَةُ بِلالاً بِأَمْرٍ سَأَلَتهُ عَنْهُ حَتى أَصبَحَ جِدًّا، فَقَامَ بِلالٌ فَآذنَهُ بِالصَّلاةِ، وتَابَعَ أَذَانَهُ، فَلَم يَخْرُجْ رَسُولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم، فَلَمَّا خَرَج صلَّى بِالنَّاسِ، فَأَخبَرهُ أَنَّ عائشَةَ شَغَلَتْهُ بِأَمْرٍ سَأَلَتْهُ عنْهُ حَتَّى أَصبحَ جِدّاً، وأَنَّهُ أَبطَأَ عَلَيهِ بالخُروجِ، فَقَال يَعْني النَّبيَّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: “إِني كُنْتُ رَكَعْتُ رَكْعْتَي الفَجْرِ”فقالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّك أَصْبَحْتَ جِدًّا؟ فقالَ:“لوْ أَصبَحتُ أَكْثَرَ مِما أَصبَحتُ، لرَكعْتُهُما، وأَحْسنْتُهُمَا وَأَجمَلْتُهُمَا” رواه أَبو دَاوُدَ بإِسناد حسن
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
196. MLANGO WA MSISITIZO WA RAKAA MBILI ZA ASUBUHI
Imepokewa kutika kwa Abû ‘Abdillâh, Bilâl bin Rabâh (Radhi za Allah ziwe juu yake) Mwadhini wa Mtume ﷺ amesimulia kuwa yeye alimwendea Mtume ﷺ ili amjulishe Swala ya asubuhi; ‘Âisha akamshughulisha Bilâl kwa jambo fulani alilomwuliza mpaka kukapambauka mno. Bilâl akainuka kwenda kumjulisha (Mtume ﷺ) na akawa anafwatisha kumjulisha. Mtume ﷺ hakutoka, alipotoka aliwaswalisha watu. Baadaye akamjulisha kuwa ‘Âisha alikuwa amemshughulisha kwa jambo fulani alilomwuliza mpaka kukapambaukiwa mno, naye akachelewa kutoka. Mtume ﷺ akamwambia: “Mimi nilikuwa nikiswali rakaa mbili za alfajiri.” Akamwambia: “Yâ Rasûlallâh, ulikuwa umepambaukiwa mno!” Akamwambia: “Lau ningalipambaukiwa zaidi ya nilivyopambaukiwa, ningaliziswali (vile vile) kwa uzuri na nikazipamba.”
[ Abû Dâwûd, isnadi yake ni Hasan. ].