١٩٥- بابُ فَضْلِ السنَنِ الراتِبِة مَعَ الفَرَائِضِ وبيانِ أَقَلِّهَا وأَكْمَلِها وما بينَهُما
وعنْ عبدِ اللَّهِ بن مُغَفَّلٍ رضِيَ اللَّه عنهُ، قَالَ: قالَ رسولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: “بَيْنَ كُلِّ أَذانَيْنِ صَلاةٌ، بيْنَ كلِّ أَذَانيْنِ صَلاةٌ، بَيْنَ كُلِّ أَذَانَيْنِ صَلاةٌ”وقالَ في الثَالثَة:”لمَنْ شَاءَ” متفقٌ عَلَيهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
195. MLANGO WA FADHILA ZA SUNNAH ZA RATIBA PAMOJA NA FARADHI, NA UBAINIFU WA UCHACHE NA UKAMILIFU WAKE NA BAINA YA HALI HIZO MBILI
Imepokewa kutika kwa Abdullâh bin Mughaffal ( Radhi za Allah ziwe juu yake ) amesema: “Mtume ﷺ amesema: “Baina ya kila adhana mbili kuna Swala, baina ya kila adhana mbili kuna Swala, baina ya kila adhana mbili kuna Swala.” Mara ya tatu akasema: “Kwa anaetaka.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim .]