باب الأمر بالمحافظة عَلَى الصلوات المكتوبات والنهي الأكيد والوعيد الشديد في تركهنَّ
وعن معاذٍ رضي اللَّه عنهُ قَالَ: بعَثني رسولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم إِلى اليَمن فَقَالَ: ” إِنَّكَ تأْتي قَوْمًا منْ أَهْلِ الكِتَابِ، فَادْعُهُمْ إِلى شَهَادةِ أَنْ لا إِله إِلاَّ اللَّه، وأَنِّي رسولُ اللَّه، فَإِنْ أَطاعُوا لِذلكَ، فَأَعْلِمهُم أَنَّ اللَّه تَعالى افْتَرَض عَلَيْهِمْ خمْسَ صَلواتٍ في كلِّ يَوْمٍ ولَيْلَةٍ، فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوا لِذلكَ، فأَعْلِمهُم أَنَّ اللَّه افْتَرَض علَيْهِمْ صَدقة تُؤْخَذُ مِنْ أَغْنِيائِهم فَتُردُّ عَلى فُقَرائِهم، فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوا لِذلَكَ، فَإِيَّاكَ وكَرائِم أَمْوالِهم وَاتَّقِ دَعْوة َالمظْلُومِ، فَإِنَّهُ لَيْسَ بَيْنَهَا وبيْنَ اللَّهِ حِجَابٌ” متفقٌ عَلَيهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
193. MLANGO WA MAAMRISHO YA KUZIHIFADHI SWALA ZA FARADHI, NA MAKATAZO YA MKAZO NA MAONYO MAKALI YA KUZIACHA
Imepokewa kutika kwa Mu‘âdh ( Radhi za Allah ziwe juu yake ) amesema: “Mtume ﷺ alinituma Yemen (ili niwe Amiri wa huko), akaniambia: “Hakika unawaendea watu ambao ni Ahlul-Kitâb. Utakapowaendea, walinganie washuhudie kuwa hakuna mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allâh, na kuwa mimi ni Mtume wa Allâh. Watakapokutii kwa hilo, wajulishe kuwa Allâh Amewafaradhia Swala tano kila mchana na usiku. Watakapokutii kwa hilo, wajulishe kuwa Allâh Amewafaradhia Zaka, inachukuliwa kutoka kwa matajiri wao na wanarudishiwa mafukara wao. Watakapokutii katika hilo, basi tahadhari mali yao yenye thamani. Na uogope dua ya mwenye kudhulumiwa, kwani hakuna pazia baina ya dua hiyo na Allâh.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim ].