0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

1069. Riyadhu Swalihina Mlango wa fadhila ya Swala ya jamaa


١٩١- باب فضل صلاة الجماعة


وعن ابنِ مسعودٍ رضي اللَّه عنهُ قال: مَنْ سَرَّه أَن يَلْقَي اللَّه تَعَالَى غداً مُسْلِمًا فَلْيُحَافِظْ عَلى هَؤُلاءِ الصَّلَوات حَيْثُ يُنادَى بهنَّ، فَإِنَّ اللَّهَ شَرَعَ لِنَبِيِّكم صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم سُنَنَ الهُدَى وَإِنَّهُنَّ مِن سُنَنِ الهُدى، وَلَو أَنَّكُمْ صلَّيْتم في بُيوتِكم كَمَا يُصَلِّي هذا المُتَخَلِّف فِي بَيتِهِ لَتَركتم سُنَّة نَبِيِّكم، ولَو تَركتم سُنَّةَ نَبِيِّكم لَضَلَلْتُم، ولَقَد رَأَيْتُنَا وَمَا يَتَخَلَّف عَنها إِلاَّ مُنَافِقٌ مَعْلُومُ النِّفَاق، وَلَقَدَ كانَ الرَّجُل يُؤتىَ بِهِ، يُهَادَي بيْنَ الرَّجُلَيْنِ حَتَّى يُقَامَ في الصَّفِّ.      رَوَاهُ مُسلِم


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



191. MLANGO WA FADHILA YA SWALA YA JAMAA


Imepokewa kutoka kwa Abdullâh bin Mas‘ûd ( Radhi za Allah ziwe juu yake ) amesema: “Anaependezewa akutane na Allâh kesho (Siku ya Qiyama) hali ya kuwa ni Muislamu, basi azihifadhi hizi Swala tano wakati zinapoadhiniwa, hakika Allâh Amemwekea Mtume wenu nyendo za uongofu, na Swala hizo ni katika nyendo za uongofu, lau nyinyi mutaswali majumbani mwenu kama huyu anaechelewa anavyoswali nyumbani mwake, mutakuwa mumeacha Sunnah ya Mtume wenu, na lau mtaacha Sunnah ya Mtume wenu, mtapotea. Kwa hakika tulikuwa tukijiona kuwa hakuna anaechelewa katika Swala hizo ila ni mtu mnafiki anaejulikana unafiki wake. Hakika, mtu alikuwa akiletwa naye anawaegemea watu wawili mpaka asimamishwe katika safu.”    [ Imepokewa na Muslim. ]


Begin typing your search above and press return to search.