١٩١- باب فضل صلاة الجماعة
وعن أبي هريرةَ رضي اللَّه عنهُ أَنَّ رسولَ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قالَ: “وَالَّذِي نَفْسِي بِيدِهِ لَقَدْ هَمَمْت أَن آمُرَ بحَطَبٍ فَيُحْتَطَب، ثُمَّ آمُرَ بالصَّلاةِ فَيُؤذَّنَ لَهَا، ثُمَّ آمُرَ رَجُلاً فَيُؤمَّ النَّاسَ ثُمَّ أُخَالِفَ إِلى رِجَالٍ فأُحَرِّقَ عَلَيْهِمْ بُيُوتَهمْ” متفقٌ عَلَيهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
191. MLANGO WA FADHILA YA SWALA YA JAMAA
Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira ( Radhi za Allah ziwe juu yake ), amepokea kuwa Mtume ﷺ amesema: “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake! Hakika nimefanya hamu niamuru zikusanywe kuni kisha niamuru kuadhiniwe kwa ajili ya Swala, halafu nimwamuru mtu awaswalishe watu, kisha niwaendee watu (wasiokuja kuswali) niwachomee nyumba zao!” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim.]