١٩١- باب فضل صلاة الجماعة
وعن أَبي هريرة رضيَ اللَّه وعنهُ قالَ: أَتَى النبيَّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم رَجُلٌ أَعمى فقَالَ: يا رسولَ اللَّهِ، لَيْس لِي قَائِدٌ يقُودُني إِلي المَسْجِدِ، فَسأَلَ رسولَ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم أَن يُرَخِّصَ لَهُ فَيُصَليِّ فِي بيْتِهِ، فَرَخَّص لَهُ، فَلَمَّا وَلىَّ دَعَاهُ فَقَالَ لَهُ: “هلْ تَسْمَعُ النِّدَاءَ بِالصَّلاةِ؟ “قَالَ: نَعَمْ، قَالَ:“فَأَجِبْ” رواه مُسلِم
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
191. MLANGO WA FADHILA YA SWALA YA JAMAA
Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira ( Radhi za Allah ziwe juu yake ) amesimulia: “Mtu mmoja kipofu alimjia Mtume ﷺ akamwambia “Yâ Rasûlallâh, mimi sina kiongozi wa kuniongoza kwenda Msikitini.” Akamwomba Mtume ﷺ amruhusu ili aswali nyumbani mwake. Akamruhusu, alipokuwa anaenda zake, Mtume ﷺ alimwita na akamwuliza: “Je, wasikia mwadhini wa Swala?” Akajibu: Ndio.” Akamwambia: “Ujibu (mwadhini).” [ Imepokewa na Muslim ]