0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

1065. Riyadhu Swalihina Mlango wa fadhila ya Swala ya jamaa


١٩١- باب فضل صلاة الجماعة


وعن أَبي هريرة رضيَ اللَّه عنهُ قَالَ: قَالَ رسولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: “صَلاةُ الرَّجُلِ في جَماعةٍ تُضَعَّفُ عَلى صلاتِهِ فِي بَيْتِهِ وفي سُوقِهِ خَمْساً وَعِشْرينَ ضِعفًا، وذلكَ أَنَّهُ إِذا تَوَضَّأَ فَأَحْسَنَ الْوُضُوءَ ثُمَّ خَرَجَ إِلى المَسْجِدِ، لا يُخْرِجُه إِلاَّ الصَّلاةُ، لَمْ يَخْطُ خَطْوةً إِلاَّ رُفِعَتْ لَه بهَا دَرَجَةٌ، وَحُطَّتْ عَنْه بهَا خَطِيئَةٌ، فَإِذا صَلى لَمْ تَزَلِ المَلائِكَة تُصَلِّي عَلَيْهِ مَا دَامَ في مُصَلاَّه، مَا لَمْ يُحْدِثْ، تَقُولُ: اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَيْهِ، اللَّهُمَّ ارحَمْهُ. وَلا يَزَالُ في صَلاةٍ مَا انْتَظَرَ الصَّلاةَ”       متفقٌ عَلَيهِ.

وهذا لفظ البخاري


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



191. MLANGO WA FADHILA YA SWALA YA JAMAA


Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira ( Radhi za Allah ziwe juu yake ) amesema: “Mtume ﷺ amesema: “Mtu kuswali kwa jamaa (ujira wake) huzidia kuswali nyumbani mwake na sokoni mwake kwa daraja zaidi ya ishirini na tano. Nako ni kuwa, mmoja wao anapotawadha kwa uzuri kisha akaenda Msikitini, hakuna kilichomtoa ela ni Swala tu, basi hatainua hatua ispokua atainuliwa daraja kwa hatua hiyo na ataondolewa dhambi kwa hatua hiyo. Na atakaposwali Malaika wataendelea kumwombea rehema maadamu yuko katika kikao chake alichoswalia maadamu hajatokwa na hadathi, wanaomba: “Ewe Mola Mswalie (Msamehe), Ewe Mola Mrehemu.” Na ataendelea kuwa katika Swala madamu anangojea Swala.”  [ Wameafikiana Bukhârî. na Muslim  ]


Begin typing your search above and press return to search.