0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

1055. Riyadhu Swalihina Mlango wa fadhila ya kutembea hadi Msikitina


١٨٩- باب فضل المشي إلى المساجد


وعن أُبَيِّ بنِ كعْبٍ رضيَ اللَّه عنه قَالَ: كانَ رجُلٌ مِنَ الأَنْصَارِ لاَ أَعْلم أَحدًا أَبْعدَ مِنَ المسْجِد مِنْهُ، وَكَانَتْ لا تُخْطِئُهُ صَلاةٌ، فَقيلَ لَهُ: لَوِ اشتَريْتَ حِمَارًا ِتَرْكَبهُ في الظَّلْمَاءِ وَفِي الرَّمْضَاءِ قالَ: مَا يَسُرُّني أَنَّ مَنْزلي إِلى جنْبِ المَسْجدِ، إِنِّي أُريدُ أَنْ يُكتَب لِي مَمْشاي إِلى المسْجِدِ، وَرجُوعِي إِذا رَجَعْتُ إِلى أَهْلي. فقالَ رسولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم:“قَدْ جَمَع اللَّه لكَ ذَلكَ كُلَّه”     رواه مسلم


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



189. MLANGO WA FADHILA YA KUTEMBEA HADI MSIKITINI


Imepokewa kutoka kwa Ubayyi bin Ka’bi ( Radhi za Allah ziwe juu yake)  amesema: “Alikuwepo mtu mmoja, sijui kama kuna mtu aliyekuwa anaishi mbali zaidi ya Msikiti kama mtu huyo, alikuwa hapitwi na Swala yoyote. Akaulizwa – au – nikamwuliza: “Waonaje lau ungalinunuwa punda utakayempanda wakati wa giza na wakati mchanga ukiwa umeshika joto?” Akajibu: “Sipendelei nyumba yangu iwepo karibu ya Msikiti, mimi nataka niandikiwe (thawabu za) kwenda kwangu Msikitini na kurejea kwangu kwa familia yangu.” Mtume ﷺ akamwambia: “Allâh Amekujumuishia yote hayo.”    [ Imepokewa na Muslim. ]


Begin typing your search above and press return to search.