١٨٨- باب فضل صلاة الصبح والعصر
وعن أَبي هُريرةَ رضي اللَّه عنهُ قالَ: قَالَ رسولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: “يَتَعَاقَبُونَ فِيكم مَلائِكَةٌ بِاللَّيْلِ، وملائِكَةٌ بِالنَّهَارِ، وَيجْتَمِعُونَ في صَلاةِ الصُّبْحِ وصلاةِ العصْرِ، ثُمَّ يعْرُجُ الَّذِينَ باتُوا فِيكم، فيسْأَلُهُمُ اللَّه وهُو أَعْلمُ بهِمْ: كَيفَ تَرَكتمْ عِبادِي؟ فَيقُولُونَ: تَركنَاهُمْ وهُمْ يُصَلُّونَ، وأَتيناهُمْ وهُمْ يُصلُّون”. متفقٌ عَلَيْهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
188. MLANGO: FADHILA YA SWALA YA ASUBUHI NA ALASIRI
Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira ( Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Mtume ﷺ amesema: “Malaika wa usiku wanapishana zamu – katika kuwahifadhi nyinyi – na Malaika wa mchana, na wanajumuika katika Swala ya asubuhi na Swala ya alasiri, kisha wanapanda wale waliokuwa nanyi, Allâh Anawauliza – Naye Anajua zaidi kuliko wao -: “Vipi mmewaacha waja Wangu?” Wanajibu: “Tuliwaacha wakiswali na tuliwaendea nao wanaswali.” [ Wameafikiana bukhari na Muslim. ]