باب النّهي عن القِرَانِ بين تمرتين ونحوهما إِذَا أكل جماعة إِلاَّ بإذن رفقته
عن جَبَلَة بن سُحَيْم، قَالَ: أصَابَنَا عَامُ سَنَةٍ مَعَ ابن الزُّبَيْرِ؛ فَرُزِقْنَا تَمْراً، وَكَانَ عبدُ الله بن عمر – رضي الله عنهما – يَمُرُّ بنا ونحن نَأكُلُ، فَيقُولُ: لاَ تُقَارِنُوا، فإنَّ النَّبِيَّ – صلى الله عليه وسلم – نَهَى عنِ القِرَانِ، ثُمَّ يَقُولُ: إِلاَّ أنْ يَسْتَأذِنَ الرَّجُلُ أخَاهُ. متفقٌ عَلَيْهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
105. MLANGO WA MAKATAZO YA KUKUSANYA TENDE MBILI NA MFANO WAKE ANAPOKULA NA WATU, ILA KWA IDHINI YA WALIOKETI NAYE
Imepokewa na Jabalah bin Suhaim amesimulia: “Tulikuja tukafikiwa na ukame pamoja na Ibnu az-Zubair, tukapata tende. ‘Abdullâh bin ‘Umar (Radhi za Allah ziwe juu yao) alikuwa akitupitia nasi tunakula, akitwambia: “Msikusanye (tende mbili pamoja), kwani Mtume ﷺ alikataza kukusanya (tende mbili pamoja), kisha akasema: “Ispokuwa mtu amwombe ruhusa nduguye.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim]