١٨٧- باب فضل الصلوات
وعَنِ ابْنِ مَسْعُودٍ رضي اللَّه عنْهُ أَنَّ رجُلاً أَصاب مِنِ امْرأَةٍ قُبْلَةً، فأَتَى النَّبِيَّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فَأَخبرهُ فأَنزَل اللَّه تَعَالَى: {وأَقِم الصَّلاةَ طَرفي النَّهَار وَزُلَفا مِنَ اللَّيْلِ، إِنَّ الْحَسنَاتِ يُذهِبْنَ السَّيِّئَاتِ} [هود: ١١٤] فَقَالَ الرَّجُلُ: أَلِيَ هَذَا؟ قَالَ:” لجمِيع أُمَّتي كُلِّهِمْ” متفقٌ عليه
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
187. MLANGO WA FADHILA ZA SWALA
Imepokewa kutoka kwa ‘Abdullâh bin Mas‘ûd ( Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia kuwa mtu mmoja alimbusu mwanamke (ambaye si halali yake), kisha akamwendea Mtume ﷺ na akamweleza habari hii. Allâh Akateremsha Aya hii: “Na simamisha Swala katika ncha mbili za mchana na nyakati za usiku zilizo karibu na mchana. Hakika mema huondoa maovu.” [11:114]. Yule mtu akauliza: “Yâ Rasûlallâh, hii ni makhsusi kwa ajili yangu tu?” Akamjibu: “Ni kwa umati wangu wote.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim ].