١٨٧- باب فضل الصلوات
وَعنْ أَبي هُرَيْرةٍ رضي اللَّه عنْهُ قَال: سمِعْتُ رسُول اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يَقُولُ: “أَرأَيْتُمْ لَوْ أَنَّ نَهْراً بِباب أَحَدِكم يغْتَسِلُ مِنْه كُلَّ يَوْمٍ خَمْس مرَّاتٍ، هلْ يبْقى مِنْ دَرَنِهِ شَيءٌ؟ “قالُوا: لا يبْقَى مِنْ درنِهِ شَيْء، قَال:”فذلكَ مَثَلُ الصَّلَواتِ الخَمْسِ، يمْحُو اللَّه بهِنَّ الخطَايا” متفقٌ عَلَيْهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
187. MLANGO WA FADHILA ZA SWALA
Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira ( Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Nimemsikia Mtume ﷺ akisema: “Niambieni lau mto utakuwa unapita katika mlango wa mmoja wenu naye anaoga humo mara tano kila siku, je, kutabakia uchafu mwilini mwake ?” Maswahaba wakamjibu: “Hapana, hangebaki na uchafu wowote” Akasema: “Huo ndio mfano wa Swala tano, Allâh Hufuta dhambi (ndogo) kwa Swala hizo.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim ]