١٨٦- باب فضل الأذان
وعنْ سَعْدِ بْن أَبي وقَّاصٍ رضِيَ اللَّه عنْهُ عَن النَّبيّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم أَنَّهُ قَالَ: “مَنْ قَال حِينَ يسْمعُ المُؤذِّنَ: أَشْهَد أَنْ لا إِله إِلاَّ اللَّه وحْدهُ لا شَريك لهُ، وَأَنَّ مُحمَّداً عبْدُهُ وَرسُولُهُ، رضِيتُ بِاللَّهِ رَبّاً، وبمُحَمَّدٍ رَسُولاً، وبالإِسْلامِ دِينًا، غُفِر لَهُ ذَنْبُهُ” رواه مسلم
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
186 – MLANGO: FADHILA YA ADHANA (KUADHINI)
Imepokewa kutoka kwa Sa’d bin Abi Waqqâs ( Radhi za Allah ziwe juu yake amempokea Mtume ﷺ kuwa amesema: “Atakayesema wakati wa kusikia mwadhini: “Ash-hadu Allâ-ilâha illallâhu wahdahû lâ sharîka lah, wa anna Muhammadan ‘abduhû warasûluh, radhîtu billâhi rabbâ wabimuhammadin rasûlâ, wabil-islâmi dînâ, [Nashuhudia kuwa hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allâh Peke Yake, na kwamba Muhammad ni Mja Wake na ni Mtume Wake, nimeridhia kuwa Allâh Ndiye Mola Mlezi, Muhammad ndiye Mtume na Uislamu ndio Dini (ya haki)_, atasamehewa dhambi zake.” [ Imepokewa na Muslim.]