١٨٦- باب فضل الأذان
وعنْ عَبْدِ اللَّه بْنِ عبدِ الرَّحْمنِ بنِ أَبي صَعْصعَةَ أَن أَبَا سعِيدٍ الخُدْرِيِّ رضِيَ اللَّه عنْهُ قَالَ لَهُ: “إنِّي أراكَ تُحِبُّ الْغَنَم والْبادِيةَ فإِذا كُنْتَ في غَنَمِكَ أَوْ بادِيَتِكَ فَأَذَّنْتَ للصلاةِ، فَارْفَعْ صَوْتَكَ بالنِّدَاءِ، فَإِنَّهُ لا يْسمعُ مَدَى صوْتِ المُؤذِّن جِنُّ، وَلاَ إِنْسٌ، وَلا شَيْءٌ، إِلاَّ شَهِد لَهُ يوْمَ الْقِيامَةِ” قَالَ أَبُو سعيدٍ: سَمِعْتُهُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم. رواه البخاري
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
186. MLANGO WA FADHILA YA ADHANA (KUADHINI)
Imepokewa kutoka kwa ‘Abdullâh bin ‘Abdurrahmân bin Abû Sa’sa‘ah amesimulia kuwa Abû Sa‘îd al-Khudry ( Radhi za Allah ziwe juu yake ) alimwambia: “Nakuona wapenda mbuzi na kwenda majangwani. Basi utakapokuwa katika mbuzi wako – au majangwani – ukaadhini kwa ajili ya Swala, nyanyua sauti yako kwa adhana. Hakika hakuna atakayesikia upeo wa sauti ya mwadhini miongoni mwa majini au wanadamu wala chochote, ispokuwa kitamtolea ushahidi Siku ya Qiyama.” Abû Sa‘îd akasema: “Maneno haya nimemsikia Mtume ﷺ .” [ Imepokewa na Bukhârî. ]