١٨٥- باب فضل الوضوء
وعنْ عُمَر بْنِ الخَطَّابِ رضي اللَّه عَنْهُ عنِ النَّبِيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قَالَ: “مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحدٍ يتوضَّأُ فَيُبْلِغُ أَو فَيُسْبِغُ الوُضُوءَ ثُمَّ يقولَ: أَشْهدُ أَنْ لا إِله إِلاَّ اللَّه وحْدَه لا شَريكَ لهُ، وأَشْهدُ أَنَّ مُحمَّدًا عبْدُهُ وَرسُولُه، إِلاَّ فُتِحَت لَهُ أَبْوابُ الجنَّةِ الثَّمَانِيَةُ يَدْخُلُ مِنْ أَيِّها شاءَ“ رواه مسلم
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
185. MLANGO WA FADHILA ZA UDHU
Imepokewa kutoka kwa ‘Umar bin al-Khattâb ( Radhi za Allah ziwe juu yake ) amesimulia: “Mtume ﷺ amesema: “Yeyote miongoni mwenu anayetawadha, akaeneza udhu wake sawasawa, kisha akasema: “Ash-hadu Allâ-ilâha illallâhu wahdahû lâ sharîka lah, wa ash-hadu anna Muhammadan ‘abduhû warasûluh, [ Nashuhudia kuwa hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allâh Peke Yake, na nashuhudia kwamba Muhammad ni Mja Wake na ni Mtume Wake_,” basi atafunguliwa milango yote minane ya Peponi, aingine katika mlango anaopenda.” [ Imepokewa na Muslim. ]
Na Tirmidhy ameongeza: “..Allâhummaj‘alnî minattawwâbîna, waj‘alnî minalmutatahhirîn, [Ewe Mola, Nijaalie miongoni mwa wenye kukubaliwa toba na Unijalie miongoni mwa wenye kujitwahirisha].”