١٨٥- باب فضل الوضوء
وعن أبي هريرةَ رضي اللَّه عنْهُ أَنَّ رسُول اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم أَتَى المقبرةَ فَقَال: “السَّلامُ عَلَيْكُمْ دَار قَومٍ مُؤْمِنينِ وإِنَّا إِنْ شَاءَ اللَّه بِكُمْ لاحِقُونَ، ودِدْتُ أَنَّا قَدْ رأَيْنَا إِخْوانَنَا”: قَالُوا: أَولَسْنَا إِخْوانَكَ يَا رسُول اللَّهِ؟ قَالَ:“أَنْتُمْ أَصْحَابي، وَإخْوَانُنَا الّذينَ لَم يَأْتُوا بعد”قالوا: كيف تَعْرِفُ مَنْ لَمْ يَأْتُوا بَعْدُ مِنْ أُمَّتِكَ يَا رَسولَ الله؟ فَقَالَ:“أَرَأَيْتَ لَوْ أَنَّ رَجُلا لهُ خَيْلٌ غُرٌّ مُحجَّلَةٌ بيْنَ ظهْريْ خَيْلٍ دُهْمٍ بِهْمٍ، أَلا يعْرِفُ خَيْلَهُ؟ “قَالُوا: بلَى يَا رسولُ اللَّهِ، قَالَ:“فَإِنَّهُمْ يأْتُونَ غُرًّا مَحجَّلِينَ مِنَ الوُضُوءِ، وأَنَا فرَطُهُمْ على الحوْضِ” رواه مسلم
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
185. MLANGO WA FADHILA ZA UDHU
Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira ( Radhi za Allah ziwe juu yake ) Mtume ﷺ amesema:” Alienda makaburini, akasema: “Amani iwe juu yenu enyi watu wa nyumba ambao ni Waislamu, hakika sisi tutakutana nanyi, Allâh Akipenda. Natamani lau tungaliwaona ndugu zetu (duniani).” Maswahaba wakamwuliza: “Kwani sisi si ndugu zako Yâ Rasûlallâh?” Akawajibu: “Nyinyi ni Maswahaba zangu, ndugu ni wale ambao bado hawajakuja.” Wakamwuliza: “Utawajua vipi watu ambao bado hawajakuja katika umati wako Yâ Rasûlallâh?” Akawaambia: “Hebu nielezeni lau mtu atakuwa ana farasi mweupe wa uso na miguu yake ni meupe yuko miongoni mwa farasi weusi tititi, je hataweza kumtambua farasi wake?” Wakajibu: “Ataweza kumtambua Yâ Rasûlallâh.” Akawaambia: “Hakika wao watakuja (Siku ya Qiyama) hali ya kuwa ni weupe wa nyuso na mikono kutokana na udhu. Nami nitawatangulia katika hodhi (ili niwatayarishie vinywaji).” [ Imepokewa na Muslim.]