0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

1028. Riyadhu Swalihina Mlango wa Fadhila za Udhu


١٨٥- باب فضل الوضوء


وعن أبي هريرةَ رضي اللَّه عنه أَنَّ رسولَ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قَالَ: “إِذا تَوَضَّأَ العبدُ المُسلِم أَوِ المؤْمِنُ فَغَسل وجهَهُ خَرجَ مِنْ وَجهِهِ كلُّ خطِيئَة نَظَر إِلَيْهَا بِعيْنيْهِ مَعَ الماءِ أَوْ معَ آخرِ قَطْرِ الماءِ، فَإِذا غَسل يديهِ، خَرج مِنْ يديهِ كُلُّ خَطيئَةٍ كانَ بطَشَتْهَا يداهُ مَعَ المَاءِ أَوْ مَعَ آخِر قَطْرِ الماءِ، فَإِذا غَسلَ رِجَليْهِ، خَرَجَتْ كُلُّ خَطِيئَةٍ مَشَتها رِجلاه مَعَ الماءِ أَوْ مَع آخرِ قَطرِ الماءِ، حَتَّى يخرُجَ نَقِيًّا مِن الذُّنُوبِ”      رواه مسلم


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



185. MLANGO WA FADHILA ZA UDHU


Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira  ( Radhi za Allah ziwe juu yake ) amepokea kutoka kwa Mtume ﷺ amesema: “Mja Muislamu au Muumini anapotawadha akaosha uso wake, litatoka – katika uso wake – kila dhambi alilolitazama kwa jicho lake pamoja na maji au pamoja na tone la mwisho la maji. Atakapoyaosha  mikono yake, litatoka kila dhambi alilolishika kwa mikono yake pamoja na maji au pamoja na tone la mwisho la maji. Atakapoyaosha miguu yake, litatoka kila dhambi aliloliendea kwa miguu yake  pamoja na maji au pamoja na tone la mwisho la maji, mpaka atoke hali ya kuwa ni safi hana dhambi.”     [ Imepokewa na Muslim.]


Begin typing your search above and press return to search.