١٨٣- باب الحثِّ عَلَى سور وآيات مخصوصة
وعن أَبي هريرة رضي اللَّه عنه قَالَ: وكَّلَني رسولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم بحِفْظِ زَكَاةِ رمضانَ، فَأَتَاني آتٍ، فَجعل يحْثُو مِنَ الطَّعام، فَأخَذْتُهُ فقُلتُ: لأرَفَعَنَّك إِلى رسُول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم، قَالَ: إِنِّي مُحتَاجٌ، وعليَّ عَيالٌ، وَبِي حاجةٌ شديدَةٌ.، فَخَلَّيْتُ عنْهُ، فَأَصْبحْتُ، فَقَال رسُولُ اللَّهِ صلَّى اللَّهُ علَيْهِ وآلهِ وسَلَّمَ:“يَا أَبا هُريرة، مَا فَعلَ أَسِيرُكَ الْبارِحةَ؟ “قُلْتُ: يَا رسُول اللَّهِ شَكَا حَاجَةً وعِيَالاً، فَرحِمْتُهُ، فَخَلَّيْتُ سبِيلَهُ. فَقَالَ:“أَما إِنَّهُ قَدْ كَذَبك وسيعُودُ”فَعرفْتُ أَنَّهُ سيعُودُ لِقَوْلِ رسُولِ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فَرصدْتُهُ. فَجَاءَ يحثُو مِنَ الطَّعامِ، فَقُلْتُ: لأَرْفَعنَّكَ إِلى رسولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم، قالَ: دعْني فَإِنِّي مُحْتاجٌ، وعلَيَّ عِيالٌ لاَ أَعُودُ، فرحِمْتُهُ فَخَلَّيتُ سبِيلَهُ، فَأَصبحتُ فَقَال لي رسُولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم:“يَا أَبا هُريْرةَ، مَا فَعل أَسِيرُكَ الْبارِحةَ؟ “قُلْتُ: يَا رسُول اللَّهِ شَكَا حَاجَةً وَعِيالاً فَرحِمْتُهُ، فَخَلَّيتُ سبِيلَهُ، فَقَال:”إِنَّهُ قَدْ كَذَبكَ وسيَعُودُ”. فرصدْتُهُ الثَّالِثَةَ. فَجاءَ يحْثُو مِنَ الطَّعام، فَأَخَذْتهُ، فقلتُ: لأَرْفَعنَّك إِلى رسولِ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم وهذا آخِرُ ثَلاثٍ مَرَّاتٍ أَنَّكَ تَزْعُمُ أَنَّكَ لاَ تَعُودُ، ثُمَّ تَعُودُ، فَقَالَ: دعْني فَإِنِّي أُعلِّمُكَ كَلِماتٍ ينْفَعُكَ اللَّه بهَا، قلتُ: مَا هُنَّ؟ قَالَ: إِذا أَويْتَ إِلى فِراشِكَ فَاقْرأْ آيةَ الْكُرسِيِّ، فَإِنَّهُ لَن يزَالَ عليْكَ مِنَ اللَّهِ حافِظٌ، وَلاَ يقْربُكَ شيْطَانٌ حتَّى تُصْبِحِ، فَخَلَّيْتُ سبِيلَهُ فَأَصْبحْتُ، فقَالَ لي رسُولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم:”ما فَعلَ أَسِيرُكَ الْبارِحةَ؟ “فقُلتُ: يَا رَسُول اللَّهِ زَعم أَنَّهُ يُعلِّمُني كَلِماتٍ ينْفَعُني اللَّه بهَا، فَخَلَّيْتُ سبِيلَه. قَالَ:“مَا هِيَ؟ “قُلْتُ: قَالَ لي: إِذا أَويْتَ إِلى فِراشِكَ فَاقرَأْ آيةَ الْكُرْسيِّ مِنْ أَوَّلها حَتَّى تَخْتِمَ الآيةَ: {اللَّه لاَ إِلهَ إِلاَّ هُو الحيُّ الْقَيُّومُ} [البقرة: ٢٥٥] وقال لِي: لاَ يَزَال علَيْكَ مِنَ اللَّهِ حَافِظٌ، وَلَنْ يقْربَكَ شَيْطَانٌ حَتَّى تُصْبِحَ. فَقَالَ النَّبِيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم:”أَمَا إِنَّه قَدْ صَدقكَ وَهُو كَذوبٌ، تَعْلَم مَنْ تُخَاطِبُ مُنْذ ثَلاثٍ يَا أَبا هُريْرَة؟ “قُلْتُ: لاَ، قَالَ:“ذَاكَ شَيْطَانٌ” رواه البخاري
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
183. MLANGO WA MAHIMIZO YA KUSOMA SURA NA AYA MAKHSUSI
Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira ( Radhi za Allah ziwe juu yake ) amesimulia: “Mtume ﷺ aliniwakilisha kuzichunga Zaka za Ramadhani. Akanijia mtu, akawa akichota chakula, nikamshika na nikamwambia: “Nitakupeleka kwa Mtume ﷺ !” Akasema: “Mimi ni mhitaji, nina watoto na nina haja kubwa.” Nikamwachia. Nilipopambaukiwa, Mtume ﷺ aliniuliza: “Ee Abû Huraira, mateka wako alifanya nini jana usiku?” Nikamjibu: “Yâ Rasûlallâh, alililia haja na watoto, nikamrehemu, nikamwachia.” Akasema: “Ama kwa kweli amekudanganya na atarudi.” Nikajua atarudi kwa kuwa Mtume ﷺ amesema hivyo. Nikamlindiza (nikamngoja), akaja akachota chakula. Nikamwambia: “Nitakupeleka kwa Mtume ﷺ !” Akaniambia: “Niache, mimi ni mhitaji na nina watoto, sitarudia tena!” Nikamrehemu na nikamwachia. Nilipopambaukiwa, Mtume ﷺ aliniuliza: “Ee Abû Huraira, mateka wako alifanya nini jana usiku?” Nikamwambia: “Yâ Rasûlallâh, amenililia haja na watoto, nikamrehemu na nikamwachia.” Akaniambia: “Kwa kweli amekudanganya na atarudi.” Nikamlindiza kwa mara ya tatu. Akaja anachota chakula, nikamshika na nikamwambia: “Nitakupeleka kwa Mtume ﷺ ! Hii ndio mara ya mwisho ya tatu, unadai kuwa hutarudi kisha unarudia!” Akaniambia: “Niache, hakika nitakufundisha maneno ambayo Allâh Atakunufaisha kwayo.” Niakamwuliza: “Ni maneno gani hayo?” Akasema: “Unapoenda kitandani mwako, soma Âyatul-Kursy, “Allâhu lâ-ilâha illâ huwalhayyulqayyûm,” mpaka uimalize Aya, kwani utaendelea kuwa una mwenye kukuhifadhi kutoka kwa Allâh, wala hakuna shetani yeyote atakayekukaribia mpaka upambaukiwe.” Nikamwachia. Nilipopambaukiwa, Mtume ﷺ aliniuliza: “Mateka wako alifanya nini jana usiku?” Nikamjibu: “Yâ Rasûlallâh, alidai kuwa atanifundisha maneno ambayo Allâh Ataninufaisha kwayo, nikamwachilia.” Akaniuliza: “Maneno gani hayo?” Nikamjibu: “Aliniambia: “Unapoenda kitandani mwako soma Âyatul-Kursy kuanzia mwanzo mpaka uimalize, “Allâhu lâ-ilâha illâ huwalhayyulqayyûm,” na akaniambia: “Utaendelea kuwa una mwenye kukuhifadhi kutoka kwa Allâh, wala hakuna shetani yeyote atakayekukaribia mpaka upambaukiwe.” Mtume ﷺ akaniambia: “Ama yeye amekwambia kweli ilihali yeye ni mwongo. Unamjua uliekuwa ukizungumza naye ee Abû Huraira siku zote hizo tatu?” Nikamjibu: “Hapana.” Akaniambia: “Huyo ni shetani.” [ Imepokelewa na Bukhârî.]
[ Imepokewa na Muslim.]