0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

1010. Riyadhu Swalihina Mlango wa Mahimizo ya kusoma sura na Aya makhsusi


١٨٣- باب الحثِّ عَلَى سور وآيات مخصوصة


وعن أَبي سعيدٍ الخُدْرِيِّ رضيَ اللَّه عنه أَنَّ رسولَ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قالَ في: {قُلْ هُوَ اللَّه أَحَدٌ} [الإخلاص: ١] ” والَّذِي نَفْسي بِيدِهِ، إِنَّهَا لَتَعْدِلُ ثُلُثَ القُرْآنِ”

وفي روايةٍ: أَنَّ رسولَ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قالَ لأَصْحابِهِ: “أَيَعْجِزُ أَحَدُكُم أَنْ يقْرَأَ بِثُلُثِ الْقُرْآنِ فِي لَيْلَةٍ”فَشَقَّ ذلكَ علَيْهِمْ، وقالُوا: أَيُّنَا يُطِيقُ ذلكَ يَا رسولَ اللَّه؟ فَقَالَ: {قُلْ هُو اللَّه أَحَدٌ، اللَّهُ الصَّمَدُ} : ثُلُثُ الْقُرْآنِ    رواه البخاري


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



183. MLANGO WA MAHIMIZO YA KUSOMA SURA NA AYA MAKHSUSI


Imepokewa kutoka kwa Abû Sa‘îd al-Khudry ( Radhi za Allah ziwe juu yake ) amesimulia: “Mtume  alisema kuhusu Sûratu Qul Huwallâhu Ahad:Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake, Sura hiyo inalingana na thuluthi ya Qur’âni.”

Riwaya nyingine imesema: “Mtume   aliwaambia Maswahaba zake: “Mmoja wenu anashindwa kusoma thuluthi ya Qur’âni katika usiku mmoja?” Jambo hilo likawa zito juu yao. Wakauliza: “Ni yupi kati yetu awezaye kufanya hivyo Yâ Rasûlallâh?” Akawaambia: “Qul Huwallâhu Ahad Allâhussamad: ni thuluthi ya Qur’âni.”     [ Imepokewa na Bukhârî.]


Begin typing your search above and press return to search.