0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

074. Riyadhu Swalihina Mlango wa Yakini na Kumtegemea Mwenyezi Mungu Hadithi ya 01

BUSTANI YA WATU WEMA

عَن ابْن عَبَّاسٍ رضي اللَّهُ عنهما قال : قال رسولُ اللَّه صلى اللَّه عليه وآله وسلم : « عُرضَت عليَّ الأمَمُ ، فَرَأيْت النَّبِيَّ وَمعَه الرُّهيْطُ والنَّبِيَّ ومَعهُ الرَّجُل وَالرَّجُلانِ ، وَالنَّبِيَّ وليْسَ مَعهُ أحدٌ إذ رُفِعَ لِى سوادٌ عظيمٌ فظننتُ أَنَّهُمْ أُمَّتِي ، فَقِيلَ لِى: هذا موسى وقومه ولكن انظر إلى الأفق فإذا سواد عظيم فقيل لى انظر إلى الأفق الآخر فإذا سواد عظيم فقيل لي : هَذه أُمَّتُكَ ، ومعَهُمْ سبْعُونَ أَلْفاً يَدْخُلُونَ الْجَنَّة بِغَيْرِ حِسَابٍ ولا عَذَابٍ » ثُمَّ نَهَض فَدَخَلَ منْزِلَهُ ، فَخَاض النَّاسُ في أُولَئِكَ الَّذينَ يدْخُلُون الْجنَّةَ بِغَيْرِ حسابٍ وَلا عذابٍ ، فَقَالَ بعْضهُمْ : فَلَعَلَّهُمْ الَّذينَ صَحِبُوا رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، وقَال بعْضهُم : فَلعَلَّهُمْ الَّذينَ وُلِدُوا في الإسْلامِ ، فَلَمْ يُشْرِكُوا باللَّه شيئاً وذَكَروا أشْياء فَخرجَ عَلَيْهمْ رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فَقَالَ : « مَا الَّذي تَخُوضونَ فِيهِ ؟ » فَأخْبَرُوهُ فَقَالَ : « هُمْ الَّذِينَ لا يرقُونَ، وَلا يَسْتَرْقُونَ ، وَلاَ يَتَطيَّرُون ، وَعَلَى ربِّهمْ يتَوكَّلُونَ » فقَامَ عُكَّاشةُ بنُ مُحْصِن فَقَالَ : ادْعُ اللَّه أنْ يجْعَلَني مِنْهُمْ ، فَقَالَ : « أنْت مِنْهُمْ » ثُمَّ قَام رَجُلٌ آخَرُ فَقَالَ : ادْعُ اللَّه أنْ يَجْعَلَنِي مِنْهُمْ فقال : «سَبَقَكَ بِهَا عُكَّاشَةُ »     متفقٌ عليه


Kutoka kwa Abdullaah bin ‘Abbaas Radhi za Allah ziwe juu yao amesema: Amesema Mtume ﷺ: [Nilionyeshwa umma mbali mbali. Nikamuona Nabii ana kipote, na Nabii mwengine ana mtu mmoja na wawili, na Nabii mwengine hana mfuasi. Mara kwa ghafla, nikaonyeshwa kundi kubwa, nikadhani kuwa ni umma wangu. Nikaambiwa: Huyu ni Musa na Kaumu yake, lakini tazama upande huu. Nikatazama, nikaona kundi kubwa. Nikaambiwa: Tazama upande mwengine. Nikaona kundi kubwa, nikaambiwa: Huu ni Umma wako, pamoja nao kuna watu sabini elfu wataingia Peponi bila hisabu wala adhabu.] Halafu akainuka na kuingia nyumbani kwake. Watu wakaanza kuzungumza na kujadiliana kuhusu wale watakaoingia Peponi bila hisabu wala adhabu. Baadhi yao wakasema: Labda hao ni wale waliosuhubiana na Mtume ﷺ. Wengine wakasema: Labda hao ni wale waliozaliwa katika Uislamu na wala hawakumshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote. Wakataja mambo mengi. Mtume ﷺ akawatokea, akawauliza: [Mlikuwa mnazungumza kuhusu nini?] Wakamueleza. Akawaambia: [Hao ni wale ambao hawazingui (hawafanyi Ruqya) wala hawataki kuzinguliwa kutoka kwa mwengine, wala hawapigi ramli na wameegemea kwa Mola wao tu.] Akasimama ‘Ukaashah bin Mihswan akasema: Muombe Mwenyezi Mungu Anijaalie katika wao. Akamwambia: [Wewe ni katika wao.] Kisha akasimama mtu mwengine, akamwambia: Muombe Mwenyezi Mungu Anijaalie miongoni mwao. Akamwambia: [Ukaasha Amekutangulia (daraja hiyo).]    [Imepokewa na Bukhaariy na Muslim]


 شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.