0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

050. Riyadhu Swalihina Mlango wa Subira Hadithi ya 26


BUSTANI YA WATU WEMA


رياض الصالحين


وَعَنْ ابْن عَبَاسٍ رضي اللَّه عنهما قال : قَدِمَ عُيَيْنَة بْنُ حِصْنٍ فَنَزلَ عَلَى ابْنِ أَخيِهِ الْحُر بْنِ قَيْسٍ ، وَكَانَ مِن النَّفَرِ الَّذِين يُدْنِيهِمْ عُمرُ رضِيَ اللَّهُ عنهُ ، وَكَانَ الْقُرَّاءُ أَصْحابَ مَجْلِسِ عُمَرَ رضي اللَّهُ عنه وَمُشاوَرَتِهِ كُهولاً كَانُوا أَوْ شُبَّاناً ، فَقَالَ عُييْنَةُ لابْنِ أَخيِهِ : يَا ابْنَ أَخِى لَكَ وَجْهٌ عِنْدَ هَذَا الأمِيرِ فَاسْتَأْذِنْ لى عَلَيْهِ ، فاستَأذنَ فَأَذِنَ لَهُ عُمرُ . فَلَمَّا دخَلَ قَالَ : هِيْ يا ابْنَ الْخَطَّاب ، فَوَاللَّه مَا تُعْطِينَا الْجَزْلَ وَلا تَحْكُمُ فِينَا بالْعَدْل ، فَغَضِبَ عُمَرُ رضيَ اللَّه عنه حتَّى هَمَّ أَنْ يُوقِعَ بِهِ فَقَالَ لَهُ الْحُرُّ : يا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ إِنَّ اللَّه تعَالى قَال لِنبِيِّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : { خُذِ الْعَفْوَ وَأْمُرْ بالْعُرْفِ وَأَعْرِضْ عَنِ الجاهلينَ }  [ سورة الأعراف: 198 ] وإنَّ هَذَا مِنَ الجاهلينَ ، وَاللَّه ما جاوَزَها عُمَرُ حِينَ تلاها ، وكَانَ وَقَّافاً

عِنْد كِتَابِ اللَّهِ تعالى     رواه البخارى


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى





Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: “’Uyaynah bin Hiswn alikuja kutoka safari, akashukia kwa mtoto wa dada yake Al-Hurri bin Qays, naye alikuwa ni katika watu ambao ‘Umar alikuwa akiwakurubisha karibu naye, wanavyuoni walikuwa ndio wa majilisi ya ‘Umar Radhi za Allah ziwe juu yake na katika watu wa ushauri wake; wawe ni wazee au vijana.Uyaynah akamwambia mtoto wa dada yake: “Ee mtoto wa dada yangu, wewe una nafasi kwa huyu Amiri, basi niombee idhini (niingie kwake).” Akamuombea idhini, ‘Umar akamruhusu. Alipoingia alisema: “Hii! Ewe mwana wa Khattwaab! Wa-Allaahi hutupatii vitu vingi, wala huhukumu kwa audilifu kati yetu.” ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akakasirika hata akataka kumuadhibu. Al-Hurru akamwambia: “Ewe Amiri wa Waumini, hakika Mwenyezi Mungu Alimwambia Nabii Wake : [Shikamana na kusamehe, na amrisha mema, na jitenge na majaahili.]   [Al-A’raaf:198]

Hakika huyu ni katika majahili. Basi Naapa kwa Mwenyezi Mungu ‘Umar hakuvuka mpaka  alipoisoma Aya hii.Na Alikuwa ‘Umar amesimama wima katika kitabu cha Mwenyezi Mungu.  [Imepokewa na Bukhari]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.