0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

05. Sahih Al-Bukhari Mlango Wa Mwanzo Wa Ufunuo (Wahyi)


صحيح البخاري


 كتاب بَدْءِ الوَحْيِ

باب كَيْفَ كَانَ بَدْءُ الْوَحْىِ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم


حَدَّثَنَا مُوسَى بْنُ إِسْمَاعِيلَ، قَالَ: حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، قَالَ: حَدَّثَنَا مُوسَى بْنُ أَبِي عَائِشَةَ، قَالَ: حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ فِي قَوْلِهِ تَعَالَى: {لاَ تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ} [القيامة: 16] قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُعَالِجُ مِنَ التَّنْزِيلِ شِدَّةً، وَكَانَ مِمَّا يُحَرِّكُ شَفَتَيْهِ – فَقَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ: فَأَنَا أُحَرِّكُهُمَا لَكُمْ كَمَا كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُحَرِّكُهُمَا، وَقَالَ سَعِيدٌ: أَنَا أُحَرِّكُهُمَا كَمَا رَأَيْتُ ابْنَ عَبَّاسٍ يُحَرِّكُهُمَا، فَحَرَّكَ شَفَتَيْهِ – فَأَنْزَلَ اللَّهُ تَعَالَى: {لاَ تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُ وَقُرْآنَهُ} [القيامة: 17] قَالَ: جَمْعُهُ لَكَ فِي صَدْرِكَ وَتَقْرَأَهُ: {فَإِذَا قَرَأْنَاهُ فَاتَّبِعْ قُرْآنَهُ} [القيامة: 18] قَالَ: فَاسْتَمِعْ لَهُ وَأَنْصِتْ: {ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ} [القيامة: 19] ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا أَنْ تَقْرَأَهُ، فَكَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَعْدَ ذَلِكَ إِذَا أَتَاهُ جِبْرِيلُ اسْتَمَعَ فَإِذَا انْطَلَقَ جِبْرِيلُ قَرَأَهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَمَا قَرَأَهُ


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ مُحَمّد بن صَالِح العُثَيْمِين رحمه الله تعالى



Sahih Al-Bukhari


Mlango wa Mwanzo wa Ufunuo (Wahyi)


Imepokewa kutoka kwa Abdullâh bin Abbâs Radhi za Allah ziwe juu yake ameelezea Neno la Allâh: “Usiuharakishe ulimi wako kwa Wahyi (unapoteremka).” Akasema: “Mtume alikuwa akipata shida wakati wa kuteremkiwa na Wahyi. Alikuwa akiiharakisha midomo yake.” ‘Abdullâh bin ‘Abbâs aeleza: “Nami nitaiharakisha midomo yangu kama alivyokuwa Mtume akiiharakisha.” Sa‘îd akasema: “Nami nitaiharakisha kama nilivyomuona ‘Abdullâh bin ‘Abbâs akiiharakisha.” Akaiharakisha midomo yake. Allâh Akateremsha: “Usiuharakishe ulimi wako kwa Wahyi (unapoteremka). Kwa hakika ni juu Yetu kukukusanyia na kukusomesha. [al-Qiyâmah: 17]. Yaani: Kuikusanyia kifuani mwako nawe usome. Wakati tunapokusomea, basi fuata kusomwa kwake. Yaani: Isikilize kwa makini. Kisha ni juu yetu kukubainishia. Yaani: Kisha ni juu yetu wewe usome. [75:16-19]. Mtume akawa baada ya hapo, anapojiwa na Jibrîl, humsikiliza, Jibril akiondoka Mtume husoma kama alivyosomewa.”.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.