BUSTANI YA WATU WEMA
وعنْ أَبي عبْدِ الرَّحْمنِ عبْدِ اللَّه بنِ مسْعُودٍ رضيَ اللَّه عنه قَال : كَأَنِّي أَنْظُرُ إِلى رسولِ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يحْكيِ نَبيّاً من الأَنْبِياءِ ، صلواتُ اللَّهِ وسَلاَمُهُ عَليْهم ، ضَرَبُهُ قَوْمُهُ فَأَدْمـوْهُ وهُو يمْسحُ الدَّم عنْ وجْهِهِ ، يقُولُ : « اللَّهمَّ اغْفِرْ لِقَوْمي فإِنَّهُمْ لا يعْلمُونَ » متفقٌ عَلَيْه
Kutoka kwa Abuu Abdir-Rahmaan, Abdulaah bin Mas’uwd Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: “Kana kwamba namuona Mtume ﷺ akieleza kuhusu Nabiy fulani, Rehema za Allah ziwe juu yao. Watu wake walimpinga na kumtoa damu usoni mwake, na huku akifuta damu kwenye uso wake huku akiomba: [Ewe Mola! Waghufurie kaumu yangu, kwani wao hawajui!] [Imepokewa na Bukhari na Muslim]