0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

796. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Sifa Ya Urefu Wa Kanzu, Mkono (Wa Kanzu Kikoi Na Ncha Ya Kilemba Na Uharamu Wa Kuburuta Sehemu Katika Mavazi…

باب صفة طول القميص والكم والإزار وطرف العمامة وتحريم إسبال شيء من ذلك على سبيل الخيلاء وكراهته من غير خيلاء


وعن أَبي جُرَيٍّ جابر بن سُلَيم رضي اللَّه عنه قَالَ: رَأَيتُ رَجلاً يصْدُرُ النَّاسُ عَنْ رَأْيهِ لاَ يَقُولُ شَيئاً إِلاَّ صَدَرُوا عَنْهُ، قلتُ: مَنْ هَذَا؟ قالوا: رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم. قلتُ: عَليكَ السَّلامُ يَا رسولَ اللَّه مَرَّتَيْنِ قَالَ: “لاَ تَقُل علَيكَ السَّلامُ، علَيكَ السلامُ تحِيَّةُ الموْتَى قُلِ: السَّلامُ علَيك”قَالَ: قلتُ: أَنتَ رسول اللَّه؟ قَالَ:“أَنَا رسول اللَّه الَّذِي إِذا أَصابَكَ ضَرٌّ فَدعَوْتَهُ كَشَفَهُ عنْكَ، وإِذا أَصَابَكَ عامُ سنَة فَدَعوْتَهُ أَنبتَهَا لَكَ، وإِذَا كُنتَ بِأَرْضٍ قَفْرٍ أَوْ فلاةٍ، فَضَلَّت راحِلَتُكَ، فَدعوْتَه رَدَّهَا علَيكَ”قَالَ: قُلْتُ: اعْهَدْ إِليَّ. قَالَ:“لاَ تسُبَّنَّ أَحداً “قَالَ: فَما سببْتُ بعْدهُ حُرّا، وَلاَ عَبْداً، وَلا بَعِيراً، وَلا شَاةً “وَلا تَحقِرنَّ مِنَ المعروفِ شَيْئاً، وأَنْ تُكَلِّمَ أَخَاك وأَنتَ مُنْبسِطٌ إِليهِ وجهُكَ، إِنَّ ذَلِكَ مِنَ المعرُوفِ. وارفَع إِزاركَ إِلى نِصْفِ السَّاقِ، فَإِن أبيتَ فَإلَى الكَعبين، وإِياكَ وإِسْبال الإِزارِ فَإِنَّهَا مِن المخِيلةِ وإِنَّ اللَّه لا يحبُّ المَخِيلة، وإن امْرؤٌ شَتَمك وَعَيَّركَ بمَا يَعْلَمُ فيكَ فَلاَ تُعيِّرهُ بِمَا تَعلَم فيهِ، فإِنَّمَا وبالُ ذلكَ عليهِ”     رواه أَبُو داود والترمذي بإِسنادٍ صحيحٍ، وَقالَ الترمذي: حديثٌ حسن صحيح.


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



119. MLANGO WA SIFA YA UREFU WA KANZU, MKONO (WA KANZU), KIKOI NA NCHA YA KILEMBA NA UHARAMU WA KUBURUTA SEHEMU KATIKA MAVAZI HAYO KWA KUFANYA KIBRI, NA KARAHA YA KUFANYA HIVYO IKIWA SI KWA KIBRI


Imepokewa na Abû Jurayyi, Jâbir bin Sulaim (Radhi za Allah ziwe juu yake)  amesimulia: Nilimuona mtu ambaye, watu walikuwa wakifwata rai yake, hasemi jambo ila na wao hulifwata. Nikauliza: “Ni nani huyu?” Wakanijibu: “Ni Mtume wa Allâh ﷺ.” Nikamwambia: “‘Alaikasalâm Yâ Rasûlallâh.” Mara mbili. Akaniambia: “Usiseme ‘Alaikassalâm, ‘Alaikassalâm ni maamkizi ya wafu. Sema: “Assalâmu ‘Alaika [Amani iwe kwako].” Nikamwuliza: “Wewe ni Mtume wa Allâh?” Akajibu: “Mimi ni Mtume wa Allâh, Allâh Ambaye, unapopatwa na madhara na ukamuomba, Atakuondolea, unapopatwa na mwaka wa ukame, ukamuomba, Atakuoteshea mimea, na unapokuwa katika nchi kame au ya jangwa, ngamia wako akapotea, ukamuomba Yeye, Atakurudishia.” Nikamwambia: “Niusie.” Akaniambia: “Usimtukane yeyote.” Basi baada ya hapo, sikumtukana yeyote, mwungwana wala mtumwa, wala ngamia wala mbuzi. “Wala usidharau chochote katika wema; na uzungumze na nduguyo nawe una bashasha umemwelekea uso wake, hakika kufanya hivyo ni katika wema, na pandisha kikoi chako hadi katika nusu ya muundi, ikiwa huwezi basi katika vifundo, nakutahadharisha usije ukaburuta kikoi, kwani kufanya hivyo ni katika kibri, hakika Allâh Hapendi kibri. Na kama mtu akikutusi na akakuaibisha kwa jambo analolijua kwako, basi wewe usimuaibishe kwa jambo unalolijuwa kwake, hakika natija mbaya ya jambo hilo, itamrudia mwenyewe.”    [ Imepokewa na Abû Dâwûd na Tirmidhy wameipokea kwa isnadi Sahîh.  Tirmidhy amesema: Hadîth hii ni Hasan Sahîh.]


Begin typing your search above and press return to search.