0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

NJIANI KUELEKEA MADINA


AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Kazi ya kuwatafuta (Mtume () na rafiki yake) ilisimama baada ya kuendelea kwa muda wa siku tatu pasina mafaniko yoyote. Mtume wa Mwenyezi Mungu na rafiki yake walijiandaa kutoka na kueleka Madina. Walikuwa wamemkodi Abdillah bin Urayqit Al-Laythy ambaye aljkuwa ni mwongozaji hodari wa njia. Alikuwa kafiri lakini walimwamini kwa hilo, walimkabidhi wanyama wao na walikuwa wameahidiana kukutana naye katika pango la Jabal Thaur, baada ya siku tatu. Akiwa na wanyama wao usiku wa Jumatatu – mwaka wa kwanza A.H – sawa na mwezi wa 9 mwaka 622 C.E. alikuja Abdullah bin Urayqiti na wanyama wawili. Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) alisema kumwambia Mtume (s.a.w), ’Ninakukomboa kwa baba yangu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (), chukua mmoja miongoni mwa wanyama wangu’, na akamsogezea aliyekuwa bora zaidi katika wao, Mtume wa Mwenyezi Mungu () akasema; ”Nakubali lakini kwa malipo.”

Asmaa binti Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) aliwapelekea chakula na akasahau kukiwekea kamba chombo chenye Chakula hicho. Walipoondoka ‘ aliamua kukitundika chombo hicho lakini hapakuwa na kamba ya‘ kufungia. Alichana ukanda wake sehemu mbili, akakitundika chombo kile, na hii ndio sababu ya kuitwa mwenye mikanda miwili. (1)

Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu () na Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) wakasafiri pamoja na ‘Amir bin Fihr pamoja na yule mwelekezaji Abdullah bin Urayqti, kwa njia ya ufukweni. Baada ya kutoka pangoni tu walielekea Kusini upande wa Yémén, kisha wakageuza na kuelekea Magharibi upande wa ufukweni, mpaka wakafika kwenye njia ambayo “watu hawajaizoea, wakaelekea upande wa Kaskazini karibu’ na Pwani ya Bahari Nyekundu. Njia hizi hazikuwa zinatumiwa na mtu yeyote isipokuwa kwa nadra sana.

Ibn Ishaq ametaja njia alizopita Mtume wa Mwenyezi Mungu (); alisema: ’-’Alipotoka nao muelekezaji, alipita pamoja nao njia ya chini ya Makka, kisha akaenda nao njia ya Pwani mpaka akaikingamia njia ya chini ya Usfana, kisha akapita nao sehemu ya chini ya mji akavuka nao mpaka akaikingamia njia ya kuvuka Qudaid. Baada ya hapo akavuka nao kutoka mahali hapo, akaenda nao Al-Kharar, ‘halafu akaenda nao Thaniyyat Al-Murra, kisha akaenda nao Laqfa, kutoka hapo akavuka nao Midlajat Laqfa, halafu akazama nao Midlajat Mujaj. Alipotoka hapo akaenda nao Marjah Majaji, halafu Marjah Akanidi, halafu Dhikashiri, ikifuatiwa na Jadaajidi, kisha Ajrad, halafu akaenda nao mpaka Dhaa Salam kafika bonde la Aadai Midlaja Taahin. Halafu akavuka nao Al- Ababid, na tena akavuka nao Al-Faja, kisha akaenda naq Thaniyyati Athir, – kuliani kwa Rakouba mpaka akafika nao Katika bonde la Riim, na baadaye Quba. (2)

Yafuatayo ni baadhi ya mambo yaliyotokea njiani:-

1. Bukhari amepokea kutoka kwa Abubakar Swiddiq (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: ”Tulikwenda usiku mzima na siku iliyofuata mpaka mchana wa jua kali sana, njia ilikuwa Tupu hapiti mtu yeyote, jiwe refu lenye kivuli ambalo halikupatwa na jua, likanyanyuliwa na tukajihifadhi katika kivuli chake. Nikamtengenezea Mtume () mahali kwa mikono yangu na nikamkunjulia ngozi ili alale hapa; Nikamwambia, ” Lala upumzike ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu () na nitakuondolea vilivyo pembezoni mwako”, Akalala. Nikatoka nikamuondolea vilivyo pembezoni mwake, ghafla katika kuzunguka kwangu nikakutana uso kwa uso namchungaji wa mbuzi akiwa anakuja na mbuzi wake kwenye lile jiwe. Akitoka kwenye jiwe mfano wa lile alipokuwa amelala Mtume () nikamwuuliza: ”Wewe ni mtumishi wa nani? Akasema, “Wa mtu mmoja katika watu wa Madina au Makka”, nikasema tena: ”Je katika mbuzi wako yupo anayetoa maziwa?” Akasema, ”Ndiyo”, nikasema: ”Je unakamua?” Akajibu, ”Ndiyo”, akamkamata mbuzi, nikamwambia, ”Kasafishe kiwele kwa kuondoa mchanga, manyoya na uchafu”, kisha akakamua katika chuchu yenye maziwa machache ndani ya chombo nilichokuwa nacho kwa ajili ya matumizi ya Mtume () ya kunywea maji na kutawadhia. Nilimwendea Mtume () nikiwa na maziwa yale lakini nikaona vibaya kumwamsha, basi niliketi karibu nae mpaka alipoamka nikayamimina maji katika chomba chenye maziwa, mpaka ikapoa sehemu yake ya’ chini, nikasema, ”Kunywa ewe Mtumbe wa Mwenyezi Mungu”, akanywa mpaka nikaridhika kuwa ametosheka, kisha akasema, “Hivi bado haujafika wakati wa safari? Nikamjibu, “Naon: umefika.” Akasema, ”Basi na twende zetu.” (3)

2. Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) alikuwa na sifa ya kuwa ni mzee maarufu anayejulikana, na Mtume () alikuwa Kijana asiyejulikana, kwa sababu hiyo kila aliyekutana nao njiani alimwuliza Abubakar: “Ni nani huyu mtu ambaye yuko mbele yako?.” Naye alikuwa akijibu kwa kusema: ”Huyu ni mtu anaeniongoza njia.” Wakadhani kuwa anakusudia njia ya kawaida, lakini alikuwa anakusudia njia ya Akhera.

3. Suraqa bin Maliki aliwafuata. Suraqa bin Maliki alisema: ”Wakati nikiwa nimekaa katika Baraza moja la jamaa zangu Banu Mudliji, alikuja mtu miongoni mwetu akatusalimia hali ya kuwa sisi tumekaa na kisha akasema; ”Ewe Suraqa nimeona kundi la watu wakipita kule ufukweni punde tu, bila shaka ni Muhammad na Masahaba zake.” Akasema Suraqa, nikajua kuwa hao ni wao, lakini nikamwambia kwa hakika hao sio wao, lakini umewaona fulani na fulani ambao wameondoka huku tukiwaona, baada ya kusema hivyo akaendelea kukaa katika lile baraza kwa muda wa saa moja zaidi na baada ya hapo, “Nikasimama na kuingia ndani na kumuamrisha mjakazi wangu aniletee farasi wangu ambaye yuko nyuma ya kichuguu ili amfunge na amuandae, wakati nikijitayarisha. Baada ya hapo nikauchukua mkuki wangu, nikatoka nao nje ya nyumba na nikaichora ardhi kwa kile chmna chake, nikainamisha sehemu yake ya juu na kisha nikamwendea farasi wangu, nikampanda, nikijua kuwa ataniwezesha kuwafikia, njiani farasi wangu alijikwaa na nikaanguka kutoka juu yake, nikasimama, nikaupeleka mkono wangu kwenye ziaka (mfuko wa kuwekea mishale) langu nikatoa vibua vya kutazamia bahati (kupigia ramli), nikatazama kwavyo bahati kwa kuviuliza, ”Je, niwadhuru au La?.” Kikatoka kile ambacho ninakichukia (kilichosema usiwadhuru). Nikampanda farasi wangu tena na. kuviasi vibua.

Farasi akaendelea kunisogeza mpaka nikafika karibu kiasi cha kusikia kisomo cha Mtume wa Mwenyezi Mungu, hali ya kuwa hageuki nyuma. Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) ndiye aliyekuwa akigeuka mara kwa mara. Ghafla miguu ya mbele ya farasi wangu ilizama katika Ardhi mpaka magotini, nikaanguka tena kutoka katika mgongo wa farasi wangu, nikamkemea akasimama lakini kidogo ashindwe kuitoa miguu yake ya mbele mahala ilipozama. Niligundua kuwa miguu yake imeathirika vibaya, tahamaki likatoka vumbi lililozagaa sehemu kubwa mfano wa moshi mzito, nikataka kujua bahati kwa vibua, kikatoka kile ambacho ninakichukia, nikalazimika kuwaita kwa kuwataka msamaha, wakasimama nikampanda farasi wangu mpaka nikawafikia.

Wakati huo nina wasiwasi mkubwa jinsi farasi alivyozamishwa ardhini kuwa litadhihiri jambo la Mjumbe wa Mwenyezi Mungu () , nikamwambia; “Kwa hakika jamaa zako wameweka zawadi kwa atakayekuuwa, na nikawaeleza khabari za mambo ambayo watu wamedhamiria kuwafanyia, na nikawataka wajiandae vizuri, hawakuniomba chochote isipokuwa waliniambia; “Uitunze siri hii.” Nikamuomba aniandikie maandishi ya amani. Alimuamrisha ‘Amir bin Fahairah naye katika karatasi ya ngozi, kisha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu () akaendelea na safari yake.3°“

Katika mapokezi mengine kutoka kwa’ Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema, ”Tulisafiri na hali ya kuwa watu wanatutafuta, Suraqa bin Maliki bin Jaatham alitukia akiwa juu ya farasi wake, nikasema, “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hawa watafutaji wamekwisha tufikia,  yeye akanijibu,

“لا تحزن إن الله معنا”

“Usihuzunike hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi.”  3°9

Akarejea Suraqa, aliwakuta watu bado wamo katika kuwatafuta, akasema, ”Kwa hakika nimekwisha kuwatafulieni khabari zilizo sahihi, bila shaka mmetoshwa na mambo yaliyopo hapa, mchana aliwatafuta kwa juhudi, na mwisho wake akawa mlinzi wao”  31°

4. Katika safari yake Mtume () alipita kwenye mahema mawili ya Ummu Maabadi Al-Khuzaiyyah. Alikuwa mwanamke aliyewashinda wenzake kwa ubora na ushujaa. Mwanamke huyo alijifunika kwa nguo yake akiwa uwanjani mwa hema, akiwalisha na kuwanywesha watu waliompitia, walimwuuliza kama alikuwa na kitu chochote cha kula?. Akajibu: “Naapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu lau kingekuwapo na kitua chochote kusingekuwa na matatizo kwenu kupewa takrima ya ugeni. Kwani wanyama hawana malisho, mwaka huu ni mwaka wa ukame.” Mjumbe wa Mwenyezi Mungu () akamuona mbuzi aliye pembezoni mwa hema akasema: ”Ni mbuzi gani huyu ewe Ummu Maabadi?’ Akasema: “Huyu ni mbuzi amebaki nyumbani kwa sababu ya maradhi hakuweza kutoka na mbuzi wengine.” Akasema, ” ]e ana maziwa?” Akasema: ”Yeye ana maradhi makubwa hawezi kuwa na maziwa.” Akasema: ”Je unaniruhusu nimkamue?’ Akasema: ”Ndiyo, ninakukomboa kwa baba yangu na mama yangu, kama unaona anatoa maziwa basi mkamue.” Mjumbe wa Mwenyezi Mungu () akapangusa kwa mkono wake kiwele chake na akamtaja Mwenyezi Mungu na akaomba, kikajaa Kiwele chake na kikatowa maziwa, akataka apelekewe chombo chake kikubwa cha kuwatosha watu wengi, akakamulia ndani yake mpaka povu likakaa juu. Akamnywesha mpaka alipotosheka na akawanywesha Masahaba zake mpaka wakatosheka, na yeye akanywa mwisho. Baada ya hapo akakamua kwa mara ya pili na kukijaza chombo, akamuachia Ummu Maabadi na wakaendelea na safari yao.

Haukupita muda mrefu mume wake Abu Maabadi akarejea kutoka machungani, hali’ ya kuwa anawachunga mbuzi wakondefu wanayumba kutokana na ukondefu, alipoyaona maziwa alistaajabu sana! kwani mbuzi hawakupata majani. Na hapana mbuzi anayefaa kwa kukamuliwa nyumbani. Mke wake akasema: ’Ninaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu, kapita mtu mwenye kubarikiwa khabari zake hivi na hivi na katika hali yake hivi na hivi – hakika mimi ninamwuona kuwa huyu ndiye yule bwana anaetafutwa na Makuraishi”, naye akasema: ”Nisifie mtu huyo alivyo ewe Ummu Maabadi.” Akamsifu kwa sifa zake ambazo ni nzuri zenye kuvutia kwa maneno yenye kuvutia kana kwamba mwenye kusikia anamwuona na yuko mbele yake. Abu Maabadi akasema: ”Naapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu huyu ni swahibu wa Makuraishi ambaye wanazungumzia khabari zake, kwa hakika ninakusudia kufuatana naye, na kwa hakika nitafanya hivyo iwapo upo uwezekano huo.”

Ikatokea sauti katika mji wa Makka watu wanaisikia na hawaoni msemaji. Sauti hiyo ikiomba:

جزى الله رب العرش خير جزائه *** رفيقين حَلاَّ خيمــتي أم مَعْبَــدِ
هـمـا نزلا بالبِـــرِّ وارتحلا به *** وأفلح من أمسى رفيق محمــد
فيا لقُصَيّ مــا زَوَى الله عنكــم *** به من فعال لا يُحَاذى وسُــؤْدُد
لِيَهْنِ بني كعـب مكــان فَتاتِهــم *** ومقعدُهـا للمؤمنـين بَمْرصَـد
سَلُوا أختكم عن شاتهـا وإنائهـا *** فإنكم إن تسألوا الشـاة تَشْـهَـــد

“Na Awalipe Mwenyezi Mungu Mola Wa Arshi ubora wa malipo yake

Marafiki wawili waliofika katika Mahema Mawili ya llmmi Maabadi;

Wao walifika kwa wema na wamesafiri kwa wema, Na amefuzu yule ambaye amekuwa ni rafiki wa Muhammad.

Enyi kina Qusway, yale ambayo Mwenyezi Mungu Ameyakusanya kutoka kwenu

Kwa sababu yake miongoni mwa Matendo hayatalipwa na ubwana.

Na iwafurahishe Banu Kaabi nafasi ya kijana wao, Na makao yao kwa Waumini kutika kuwalindilia

Muulizeni dada yenu kuhusu Mbuzi wake nu chombo chake

Kwa hakika kama nyinyi mtamuuliza Mbuzi kuhusu khabari hizo, atashuhudia.”

Asmaa (Radhi za Allah ziwe juu yake) alisema hatukujua ni wapi ameelekea Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (), ghafla alikuja mtu mmoja katika majini-, kutokea ya Makka, akaimba beti hizi na hali ya kuwa watu wanamfuata na wanamsikiei sauti yake na hawamuoni, mpaka akatoka Makka. amesema, ”Tuliposikia kauli yake, tulielewa mahali alipo elekea Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alielekea Madina (5)

5. Alipokuwa njiani Mtume () alikutana na Aba Buraida, ambaye alikuwa ni kiongozi wa jamaa zake, alitoka katika kumtafuta Mtume () na Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwa kutaraji kufanikiwa kwa kupata zawadi kubwa ambayo Makuraishi wameitangaza. Alipomkabili Mjumbe wa Mwenyezi Mungu () na kuzungumza naye, alisilimu pale pale, pamoja na watu sabini katika jamaa zake. Kisha akavua kilemba chake na akakifunga katika mkuki wake, akakifanya kuwa ni bendera; bendera ambayo ilitangaza kuwa Mfalme wa amani na salama amedhihiri ili aijaze dunia uadilifu na usawa. (6).

6. Njiani Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alikutana na Al- Zubair hali yakuwa yumo katika msafara wa Waislamu, wafanyabiashara waliokuwa wakirejea kutoka Sham, akamvalisha nguo nyeupe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu () na Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake). (7)


1)  Sahihil Bukhari, Juzuu 1, Uk. 533, 555. Ibn Hisham, Iuzuu 1, Uk. 486.
2) Ibn Hisham, Juzuu 1, Uk. 491,492.
3) Ibid. luzuu 1, Uk 554. Zilad Mll’ad, Iuzuu 2
4) Sahihul Bukhari, Iuzuu 1, Uk. 516. 31 Zaad Mu’ad, Iuzuu 2, Uk. 53. 303 i Z}
5) Zaad Ma’ad, Iuzuu 2, Uk. 53-54. 311 
6) Rahmatun Lil ‘Alamin, Iuzuu 1, Uk. 101.
7) Sahihil Bukhari, Iuzuu 1, Uk. 554. 306

Begin typing your search above and press return to search.