0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MWANZO WA MAZUNUMZO NA UFAFANUZI WA ABBAS KUTOKANA NA UKUMBWA WA JUKUMU.


AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Baada ya kikao kukamilika yalianza mazungumzo kwa kuupitisha mwafaka wa kidini na kijeshi, na mzungumzaji wa kwanza alikuwa ni ’Abbas bin Abdil Muttwalib, ammi wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) ambaye alizungumza ili kuwawekea wazi ukubwa wa jukumu ambalo watakabidhiwa, ikiwa ni matokeo ya muafaka huu, akasema: ”Enyi jamaa katika Khazraji! (na walikuwa Waarabu wanawaita Answanfi – Khazraji — wale ambao ni Khazraji na wale ambao ni Ausi wote wawili) kwa hakika nyote mnafahamu nafasi aliyonayo Muhammad kwetu sisi. Kwa hakika tumemhami dhidi ya jamaa zetu walio bado katika shirki, kwa hivyo yeye yuko katika nguvu za jamaa zake na kinga katika mji wake. Kwa hakika yeye amewakataa watu wake na anataka kuwaegemeeni na kujiunga nanyi, ikiwa mnaona kuwa mtamtekelezea lile ambalo mmemwita kwalo na kuwa mtamlinda na wale wanaompinga. Basi mnaachwa mbebe jukmnu hilo, na kama mtaona kuwa nyinyi mtamtoa na mtamwachia baada ya kumchukua na kwenda naye kwenu basi tokea sasa mwacheni, kwani yeye yumo katika ulinzi na himaya ya jamaa zake na mji wake.” Ka’ab amesema tukamwambia, “Tumeyasikia yale ambayo umeyasema, zungmnza ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) na chukua kwa ajili yako binafsi na Mola Wako lile ambalo unalipenda (1) Jibu hili linatufahamisha hali waliyokuwa nayo, misimamo thabiti, azma, ushujaa, imani na ikhlasi zao katika kulibeba jukumu hili kubwa na kuyakubali matokeo yake yenye hatari.

Baada ya hapo Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) akatoa ufafanuzi wake, na kisha makubaliano yakakamilika.

Vifungu vya Mkataba:

Imam Ahmad ameyapokea haya kutoka kwa Jabir (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwa ufafanuzi. Jabir (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema;

قلنا : يا رسول الله ، علام نبايعك ؟ قال : تبايعوني على السمع والطاعة في النشاط والكسل ، وعلى النفقة في العسر واليسر ، وعلى الأمر بالمعروف والنهي عن المنكر وأن تقولوا في الله ، لا يأخذكم في الله لومة لائم ، وعلى أن تنصروني إن قدمت عليكم يثرب ، وتمنعوني مما تمنعون منه أنفسكم وأزواجكم وأبناءكم ولكم الجنة . فقلنا : نبايعك

”Tulimuuliza‘ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) tunakupa ahadi kwa jumbo gimi?’ Akujibu: ”Kwanza, Kunisikiliza nu kunitii wakati wote wa uchangamfu na wakati wa uvivu. Pili, Kutoa mali wakati wa uzito na wepesi. Tutu, Kuamrisha mema na kukataza maovu. Nne, Kuwa mtasimamia majukumu kwa ajili ya Allah (ﷻ) bila kujali lawama ya mwenye kulaumu. Tano, Na kuwa mtaninusuru wakati nitakapofika kwenu Yathrib na kunikinga kwa yale mnayojikinga kwa ajili ya nafsi zenu na wake zenu na watoto wenu , nu nyinyi kwa ajili hiyo mtapata pepo.  Tukasema Tumekupa ahadi “2“

Katika mapokezi ya Ka’ab, kutoka kwa Ibn Ishaq, kifungu cha mwisho kafika vifungu hivi alisema: Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) akazungumza na baadaye akasoma Qur’an na akawakumbusha watu umuhimu wa Kumtii Mwenyezi Mungu (ﷻ) na akawataka waingie kwenye Uislamu. Kisha akasema: ”Ninapeana ahadi na nyinyi kuwa mtanikinga na kile ambacho mnanajikinga nacho wake zenu na watoto wenu”, Baraa bin Ma’arour akaukamata mkono wake na akasema: ”Ndiyo ninaapa kwa yule ambaye amekuleta kwa ukweli (kama Mtume) kwa hakika tutakulinda na tunachojilinda nacho, tunakuomba upeane ahadi na sisi, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w). Tunaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, sisi ni watu wa vita na ni watu wa misimamo, tumeyarithi yote kutoka kwa mababu zetu.” Abu Haytham bin Tayhani akayaingilia maneno haya na hali yakuwa Baraa bado anazungumza na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na akasema: ”Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ); Kwa hakika kati yetu na jamaa zetu wapo watu ambao wanaweza kuivunja ahadi hii (akiwakusudia Mayahudi). Hivi iwapo sisi tutafanya hivyo kisha Mwenyezi Mungu (ﷻ) Akakupa mafanikio, utarejea kwa watu wako na kutuacha?.” Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) akatabasamu na akasema: ‘Isipokuwa damu kwa damu na ubomoaji kwa ubomoaji Mimi ni miongoni mwenu na nyinyi ni miongoni mwangu, nitapiguna vita na yule ambaye mnapigana naye na nitafunya amani na yule ambuye mnafanya naye amani (3)

Kutilia Mkazo Uzito wa Mkataba.

Baada ya kukamilika kwa mazungumzo kuhusu mashati ya mkataba na kukubaliana namna ya utaratibu wa utekelezaji wake, walisimama watu wawili kutoka katika kundi la kwanza midngoni mwa wale waliosilimu wakati wa msimu wa kumi na moja na kumi na mbili wa Utume, na alisimama mtu mwingine, wote walisisitizia ukubwa wa jukumu lao, ili wasije wakapeana naye ahadi na kula kiapo kwa jambo ambalo bado halijawa wazi kwao, na ili wajue kiwango cha maandalizi yanayotakiwa na kujitoa muhanga na wawe na uhakika na jambo hilo.

Ibn Ishaq amesema: ”Walipokutana kwa madhumuni ya kutoa ahadi ‘Abbas bin ‘Ubada bin Nadhla aliwauliza, ”Je mnajua bmnapeana ahadi kwa jambo gani na mtu huyu?.” Wakajibu, ”Ndiyo.” Akasema: “Kwa hakika nyinyi mnapeana naye ahadi ya kushirikiana naye katika kazi yake ya kutangaza Dini, na kumpiga vita adui yeyote, awe mwekundu au mweusi katika watu kama mtaona kuwa ipo haja ya kufanya hivyo kwa hofu ya kuteketezewa mali zenu, au mkiwaona watukufu wenu wanauliwa mtamwachia na kumtoa kwa adui?. Hili lisemeni kutokea sasa, hata hivyo; Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu iwapo mtalifanya jambo hilo basi huo ni udhalili wenu wa duniani na kesho akhera. Kama mnaona kuwa nyinyi mtamtekelezea lile mlilomwitia, hata kwa kuteketezwa mali na kuuliwa kwa Watukufu wenu mchukuweni. Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, kwa hakika kumnchukua kwenu ndio jambo la kheri kwenu hapa duniani na kesho akhera.” Wakasema; “Kwa hakika sisi tunamchukua bila ya kujali kuteketezwa kwa mali au kuuliwa kwa Watukufu wetu. Tutapata nini, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) sisi tukikutekelezea hilo?.” Akawajibu; ”Mtapata pepo.” Wakamwambia, ”Unyooshe mkono wako, akaukunjua mkono wake wakampa ahadi ya ut-ii.

Katika mapokezi ya Jabir (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema; ”Tukasimama na tukatoa ahadi, wakati huo As’ad bin Zurarah amekamatwa mkono wake – na hali ya kuwa yeye ni mdogo zaidi wa Wale watu sabini waliokuwepo.” Akasema; “Taratibuni enyi watu wa Yathrib, kwa hakika sisi hatukusafiri kwa ngamia kuja huku kwa madhumuni ya kuja kwake, ila ni baada ya kuelewa kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷻ). Tokea leo, hili lizingatiwe kuwa ni kutengana na Waarabu wote na kuuliwa kwa wabora wetu, na kuwakateni nyinyi panga. Kama mko tayari kuyavumilia hayo mchukuweni na malipo yenu yako kwa Mwenyezi Mungu (ﷻ). Iwapo nyinyi mna hofu juu ya nafsi zenu, hofu kubwa, basi mwacheni, maana hilo ni udhuru wa kutosha kwenu mbele ya Mwenyezi Mungu (ﷻ).

Kiapo cha Ahadi ya Utii

Baada ya kupitishwa vifungu vya mkataba na baada ya mkazo na kusisitizwa umuhimu wa jambo lenyewe, Mkataba ulianzwa kufungwa kwa kupeana mikono. Jabir (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema; “Baada ya kuyazungumzia maneno ya As’ad, bin Zurarah; wakasema Ewe As’ad. tuondolee mkono wako, tunaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu (ﷻ) kuwa hatuuachi mkataba huu na hatutauvunja.

Wakati huo ndio As’ad alielewa kiwango cha maandalizi ya wale watu kwa ajili ya kujitoa muhanga katika njia ya Dini. Kutokana na hilo akapata uhakika wa kuungwa mkono, hasa kwa vile yeye ndiye aliyekuwa mlinganiaji mkubwa pamoja na Mus’ab bin ’Umair (Radhi za Allah ziwe juu yake) na kwa kawaida yeye ndiye aliyekuwa kiongozi wa Kidini wa hawa waliokuwa wanatoa ahadi, yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoa ahadi hii.

Ibn Ishaq alisema; ”Banu Najjari wanadai kuwa Abu As’ad bin Zurarah ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kumpa mkono wa utii Mtume (ﷺ), na baada yake wengine wakafuata katika kutoa ahadi zao.”

Jabir (Radhi za Allah ziwe juu yake) alisema, ”Tukasimama mbele yake mtu mmoja baada ya mwingine, akapokea ahadi kutoka kwa kila mmoja wetu, naye akimbashiria pepo kila aliyetoa ahadi.

Ama kuhusu ahadi ya wale wanawake wawili ambao walishuhudia tukio hilo, ahadi yao ilitolewa kwa matamko tu bila ya kupeana mikono, kwani Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) hakuwa na tabia ya kuwapa mkono wanawake ajnabi, isipokuwa wakeze na binti zake_. (4)

Viongozi Kumi na Wawili

Baada ya kukamilika kwa mkataba, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alitaka kuchaguliwa kwa viongozi kumi na wawili watakaokuwa wasimamizi wa jamaa zao, na watakaobeba majukumu ya kuhakikisha utekelezwaji wa vifungu vya mkataba. Aliwaambia watu waliokuwa wamekusanyika pale, ”Nichagulieni kutoka miongoni mwenu viongozi kumi na wawili ili wawe wasimamizi wa jamaa zao, kwa yale mambo ambayo yako kwao.” Uchaguzi ukafanyika na wakati ule ule wakachaguliwa watu tisa kutoka upande wa Khazraji na watatu kutoka upande wa Ausi, kama ifuatavyo: –

Viongozi Kutoka Upande wa Khazraji

1. As’ad bin Zurarah bin Adas

2. Sa’ad bin Rabia bin ’Amru

3. Abdullah bin Rawaha bin Tha’alaba

4. Rafii bin Malild bin A1-Ajilan

5. Al-Baraa bin Maarour bin Swakhri

6. Abdullah bin ’Amru bin Hiram

7. ’Ubada bin Swamiti bin Qaysi

8. Sa’ad bin ’Ubada bin Dolaym

9. Al-Mundhiri bin ’Amru bin Khunaysi

Viongozi Kutoka Upande wa Ausi

1. ’Usaid bin Khudhair bin Simaki

2. Sa’ad bin Khaithama bin Harithi

3. Rifaa bin Abdul A1- Mundhir bin Zubair. (5)

Baada ya uchaglwi kukamilika, Mtume (ﷺ) alichukua ahadi nyingine kutoka kwao kwa ile sifa yao ya kuwa viongozi ambao wangewajibika. Aliwaambia; ”Nyinyi ni wadhumini wa yule yaliyo kwa jamaa zenu kama walivyopewa dhamana wafuasi wa Isa mwana wa Mariam na mimi ni mdhamini juu ya Waislamu wote.” Wote wakaitikia, ”Ndiyo.”


1) Ibn Hisham, Iuzuu 1, Uk. 440-441
2) Imam Ahmad, imesahihishwa na Al-Hakim na Ibn Hibban (Angalia Mukhtasar Siratu Rrasul, Uk. 155; na llm Hisham, Iuzuu 1, Uk. 454).Arrahiq Al-Makhtuum Uk -265-266
3) Ibn Qutayba amesema, ‘Wakati wa kufanya mikataba ya kunusuriana na kusaidiana au mikataba ya ujirani, Waarabu walikuwa na msemo waliopenda kuutumia; damu yangu ni damu yako na kubomoa kwako ni kubomoa kwangu-maana yake-huu ni mshikamano wa kidugu. (Wafasiri) 1“ Ilm Hislmm, juzuu 1, Uk. 442. 269
4) Sahihi Muslim Juzuu 2, Uk 131
5) Ibnu Hisham, juzuu 1, Uk. 443-444, 446.

Begin typing your search above and press return to search.