0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

346. Riyadhu Swalihina Mlango wa Kuwakirimu watu wa Nyumba ya Mtume ﷺ (Ahlulbayt) na kubainisha Ubora wao

باب إكرام أهل بيت رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – وبيان فضلهم


وعن يزيد بن حَيَّانَ، قَالَ: انْطَلَقْتُ أنَا وحُصَيْنُ بْنُ سَبْرَة، وَعَمْرُو ابن مُسْلِم إِلَى زَيْد بْنِ أرقَمَ رضي الله عنهم ، فَلَمَّا جَلسْنَا إِلَيْهِ قَالَ لَهُ حُصَيْن: لَقَدْ لقِيتَ يَا زَيْدُ خَيْراً كَثِيراً، رَأيْتَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -، وسمعتَ حديثَهُ، وغَزوْتَ مَعَهُ، وَصَلَّيْتَ خَلْفَهُ: لَقَدْ لَقِيتَ يَا زَيْدُ خَيْراً كَثيراً، حَدِّثْنَا يَا زَيْدُ مَا سَمِعْتَ مِنْ رسولِ الله – صلى الله عليه وسلم – قَالَ: يَا ابْنَ أخِي، وَاللهِ لقد كَبِرَتْ سِنِّي، وَقَدُمَ عَهدِي، وَنَسيتُ بَعْضَ الَّذِي كُنْتُ أعِي مِنْ رسولِ الله – صلى الله عليه وسلم -، فما حَدَّثْتُكُمْ، فَاقْبَلُوا، ومَا لا فَلاَ تُكَلِّفُونيهِ. ثُمَّ قَالَ: قام رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – يَوماً  فينا خَطِيباً بمَاء يُدْعَى خُمَّاً بَيْنَ مَكَّةَ وَالمَدِينَةِ، فَحَمِدَ الله، وَأثْنَى عَلَيهِ، وَوعظَ وَذَكَّرَ، ثُمَّ قَالَ: {أمَّا بَعدُ، ألاَ أَيُّهَا النَّاسُ، فَإنَّمَا أنَا بَشَرٌ يُوشِكَ أنْ يَأتِي رسولُ ربِّي فَأُجِيبَ، وَأنَا تارك فيكم ثَقَلَيْنِ: أوَّلُهُمَا كِتَابُ اللهِ، فِيهِ الهُدَى وَالنُّورُ، فَخُذُوا بِكتابِ الله، وَاسْتَمْسِكُوا بِهِ}، فَحَثَّ عَلَى كِتَابِ الله، وَرَغَّبَ فِيهِ، ثُمَّ قَالَ: {وَأهْلُ بَيْتِي أُذكِّرُكُمُ الله في أهلِ بَيْتي، أذكرُكُمُ الله في أهل بيتي} فَقَالَ لَهُ حُصَيْنٌ: وَمَنْ أهْلُ بَيتهِ يَا زَيْدُ، أَلَيْسَ نِسَاؤُهُ مِنْ أهْلِ  بَيْتِهِ؟ قَالَ: نِسَاؤُهُ مِنْ أهْلِ بَيتهِ، وَلكِنْ أهْلُ بَيتِهِ مَنْ حُرِمَ الصَّدَقَةَ بَعدَهُ، قَالَ: وَمَنْ هُمْ؟ قَالَ: هُمْ آلُ عَلِيٍّ وَآلُ عقيل وَآلُ جَعفَرَ وآلُ عَبَّاسٍ. قَالَ: كُلُّ هؤلاء حُرِمَ الصَّدَقَةَ؟ قَالَ: نَعَمْ

رواه مسلم

وفي رواية: {ألاَ وَإنّي تَارِكٌ فِيكُمْ ثَقَليْنِ: أحَدُهُما كِتَابُ الله وَهُوَ حَبْلُ  الله، مَنِ اتَّبَعَهُ كَانَ عَلَى الهُدَى، وَمَنْ تَرَكَهُ كَانَ عَلَى ضَلالَة}


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Yazîd bin Hayyân amesimulia: “Mimi, Husain bin Sabrah na ‘Amru bin Muslim, tulimtembelea Zaid bin Arqam Radhi za Allah ziwe juu yao. Tulipokuwa tumeketi naye, Husain akamwambia: “Ee Zaid, umepata kheri nyingi, umemuona Mtume , ukasikia mazungumzo yake, ukapigana Jihadi pamoja naye na ukaswali nyuma yake. Hakika umepata kheri nyingi ewe Zaid! Tuhadithie Zaid uliyosikia kwa Mtume !” Zaid akamwambia: “Ee mpwa wangu! Wallahi umri wangu umekuwa mkubwa, zama zangu zimepita na nimeyasahau baadhi nilioyahifadhi kutoka kwa Mtume . Nitakachowazungumzia kipokeeni, na ambacho sikuwahadithia musinilazimishe kukizungumza.” Kisha akasema: “Siku moja Mtume alituhutubia sehemu inayoitwa Khum; baina ya Makkah na Madina; akamhimidi Allâh, akamsifu, akatoa waadhi, akakumbusha kisha akasema: “Ama baada ya haya. Fahamuni enyi watu! Hakika mimi ni mwanadamu, Mjumbe wa Mola wangu anakaribia kunijia nami niitike mwito wake, nami nimewaachia vizito viwili; cha kwanza ni Kitabu cha Allâh, ndani yake muna uongofu na nuru, chukueni Kitabu cha Allâh na mshikamane nacho. Akasisitiza mno juu ya kushikamana na Kitabu cha Allâh. Kisha akasema: Na watu wa nyumba yangu. Nawakumbusha Allâh katika watu wa nyumba yangu, nawakumbusha Allâh katika watu wa nyumba yangu. Husain akamwuliza: Ni nani hao watu wa nyumba yake ewe Zaid? Wake zake si ni katika watu wa nyumba yake? Akamjibu: Wakeze pia ni katika watu wa nyumba yake. Lakini watu wa nyumba yake (hasa) ni wale walioharamishiwa sadaka baada yake. Akauliza: Ni nani hao? Akamjibu: Wao ni familia ya Alî, familia ya Aqîl, familia ya Jafar na familia ya Abbâs. Akamwuliza: Wote hao wameharamishiwa sadaka? Akamjibu: Ndio.   [Imepokewa na Muslim.]

na katika Riwaya nyingine imesema Mtume akasema): [Fahamuni! Hakika nimewaachia vizito viwili; kimojawapo ni Kitabu cha Allâh, nacho ni kamba ya Allâh, mwenye kukifwata atakuwa yu katika uongofu, na mwenye kukiacha atakuwa katika upotevu.]


Begin typing your search above and press return to search.