0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

326. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Kuwafanyia Wema Wazazi Na Kuunga Kizazi (Undugu) 16

باب بر الوالدين وصلة الأرحام


وعن زينب الثقفيةِ امرأةِ عبدِ الله بن مسعود رضي الله عَنْهُ وعنها، قَالَتْ: قَالَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -: {تَصَدَّقْنَ يَا مَعْشَرَ النِّسَاءِ وَلَوْ مِنْ حُلِيِّكُنَّ}، قَالَتْ: فَرَجَعْتُ إِلَى عبد الله بنِ مسعود، فقلتُ لَهُ: إنَّكَ رَجُلٌ خَفِيفُ ذَاتِ اليَدِ، وَإنَّ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – قَدْ أمَرَنَا بِالصَّدَقَةِ فَأْتِهِ، فَاسألهُ، فإنْ كَانَ ذلِكَ يْجُزِىءُ عَنِّي وَإلاَّ صَرَفْتُهَا إِلَى غَيْرِكُمْ. فَقَالَ عبدُ اللهِ: بَلِ ائْتِيهِ أنتِ، فانْطَلَقتُ، فَإذا امْرأةٌ مِنَ الأنْصارِ بِبَابِ رسولِ الله  – صلى الله عليه وسلم – حَاجَتي حَاجَتُها، وَكَانَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – قَدْ أُلْقِيَتْ عَلَيهِ المَهَابَةُ، فَخَرجَ عَلَيْنَا بِلاَلٌ، فَقُلْنَا لَهُ: ائْتِ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -، فَأخْبرْهُ أنَّ امْرَأتَيْنِ بالبَابِ تَسألانِكَ: أُتُجْزِىءُ الصَّدَقَةُ عَنْهُمَا عَلَى أزْواجِهمَا وَعَلَى أيْتَامٍ في    حُجُورِهِما؟، وَلاَ تُخْبِرْهُ مَنْ نَحْنُ، فَدَخلَ بِلاَلٌ عَلَى رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -، فسأله، فَقَالَ لَهُ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -: {مَنْ هُمَا؟} قَالَ: امْرَأةٌ مِنَ الأنْصَارِ وَزَيْنَبُ. فَقَالَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -: يُّ الزَّيَانِبِ هِيَ؟}، قَالَ: امْرَأةُ عبدِ الله، فَقَالَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -: {لَهُمَا أجْرَانِ: أجْرُ القَرَابَةِ وَأجْرُ الصَّدَقَةِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.


متن الحديث



Imepokewa kutoka Zainab ath-Thaqafiyyah mkewe ‘Abdullâh bin Mas‘ûd Radhi za Allah ziwe juu yake amesimulia: “Mtume alitwambia: “Enyi mkusanyiko wa wanawake, toeni sadaka japo katika dhahabu zenu.” Nikamwendea ‘Abdullâh bin Mas‘ûd, nikamwambia: “Wewe huna mali, na Mtume ametuamuru kutoa sadaka, nenda ukamwulize. Ikiwa nitakachowapa kitanitosheleza (kuwa nimetoa sadaka) nitawapa nyinyi, la si hivyo nitawapa wengine.” ‘Abdullâh bin Mas‘ûd akamwambia: “Bali mwendee wewe.” Nikamwendea, nikamuona mwanamke wa ki-Ansari yuko mlangoni mwa Mtume , haja yangu ni kama haja yake. Mtume alikuwa ni mtu aliepewa haiba (utisho). Bilâl akatutokea, tukamwambia: “Mwendee Mtume umweleze kuwa wanawake wawili walioko mlangoni wanakuuliza: Itawatoshea wao kutoa sadaka kuwapa waume zao na mayatima walio katika malezi yao? Wala usimwambie kuwa sisi ni akina nani.” Bilâl akamwendea Mtume , akamwuliza. Mtume akamwuliza: “Ni akina nani hao?” Akamjibu: “Ni mwanamke katika Ansari na Zainab.” Mtume akauliza: “Zainabu yupi huyo?” Akajibu: “Mke wa ‘Abdullâh.” Mtume akasema: [ Watapata ujira mara mbili: ujira wa kizazi (undugu/uhusiano) na ujira wa kutoa sadaka.”]   [Wameafikiana Bukhari na Muslim]


Begin typing your search above and press return to search.