KITAAB AT-TAWHIID
باب (11) من الشرك: النذر لغير الله
وقول الله تعالى: {يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْماً كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيراً} الإنسان:7
وقوله: {وَمَا أَنْفَقْتُمْ مِنْ نَفَقَةٍ أَوْ نَذَرْتُمْ مِنْ نَذْرٍ فَإِنَّ اللَّهَ يَعْلَمُهُ} البقرة:270
وفي الصحيح عن عائشة رضي الله عنها: أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: [من نذر أن يطيع الله فليطعه ; ومن نذر أن يعصي الله فلا يعصه] رواه البخاري
فيه مسائل:
الأولي: وجوب الوفاء بالنذر
الثانية: إذا ثبت كونه عبادة الله، فصرفه إلى غيره شرك
الثالثة: أن نذر المعصية لا يجوز الوفاء به
MLANGO WA 11 KUWEKA NADHIRI KWA ASIYEKUWA MWENYEZI MUNGU NI SHIRKI
Na kauli ya Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Wanatimiza ahadi,na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana,] [Al-Insaan: 7]
Na kauli Yake ﷻ :
[Na chochote mnacho toa au nadhiri mnazo weka basi hakika Mwenyezi Mungu anajua.] [Al-Baqarah: 270]
Na katika Asw-Swahihi: Imepokelewa kutoka kwa ‘Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwamba Mtume ﷺ amesema: [Atakayeweka nadhiri kumtii Mwenyezi Mungu na amtii. Na atakayeweka nadhiri kumuasi Mwenyezi Mungu basi asimuasi] [Imepokewa na Bukhari]
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1. Uwajibu wa kutekeleza nadhiri.
2. Ikiwa imethibitika kuwa nadhiri Ibada ya Mwenyezi Mungu ﷻ, basi kumfanyia mwengine ni shirki.
3. Kwamba nadhiri ya masia haifai kutekeleza.