KUHAMA KWA ‘UMAR (R.A.) KUELEKEA MADINAH
Muda yalipozidi maudhi ya Maquraish juu ya waislamu. na wakaruhusiwa kuhamia Yathrib (Madinah), walianza kuhamia huko kwa siri huku wakijificha isipokuwa ‘Umar (r.a.). Imepokewa kuwa: ‘Ali ibn Abi Talib (r.a.) kuwa amesema:”Sifahamu kuwa kuna yoyote katika waliohama kuelekea Madinah isipokuwa amehama kwa siri isipokuwa ‘Umar (r.a.) alipoazimia kuhama alichukua upanga wake na akavaa upinde wake, na akabeba mikononi mwake mishale, akaelekea mpaka Al-Ka’ba na mabwenyenye wa Kiquraish walikuwa wamekaa pembeni mwa Al- Ka’ba. Na alitufu mara saba kwa makini. Baada ya kutufu ‘Umar (r.a.) akasali katika Maqamu Ibrahim, kisha akasimama katika kila kikundi cha Maquraish na kuwaambia:
[شاهت الوجوه ، من أراد أن تثكله أمه و يوتم ولده و يرمل زوجته ، فليلقني وراء هذا الوادي]
[Nyuso zenu ni mbaya, basi mwenye kutaka akoswe na mama yake, na kuwafanya mayatima watoto wake, na kumfanya mjane mke wake, akutane nami nyuma ya bonde hili.]
Kisha akaelekea Madinah, na wala hakuna yoyote aliyemfuata. Na walihama pamoja naye baadhi ya wanyonge.
*Khulafaau Arrashinun Uk 61