EWE ALI, WEWE KWANGU NI KAMA MFANO WA HARUNI KWA MUSA
Katika shubuhati za mashia katika kuitetea itakadi yao ya Uimamu ni hadithi ya Bwana Mtume alipomwambia Sayyidna Ali Radhi za Allah ziwe juu yake,
[يا علي أنت مني بمنزلة هارون من موسى إلا أنه لا نبي بعدي] رواه البخاري ومسلم
[Ewe Ali, wewe kwangu mimi, ni kama cheo cha Haruun kwa Musa ila tu hakuna Nabii baada yangu]
Mashia wanadai kwa Hadithi hii, kuwa Sayyidna Ali radhi za Allah ziwe juu yake ndie anaestahiki wilaya na Ukahlifa baada ya kufa Mtume ﷺ .
Jawabu:
1. Bila shaka hadihti hii ni swahihi na Imepokelewa na Bukhari na Muslim na wengineo katika wanachuoni wa hadithi,ndio wanachuoni wakiweka katika fadhila za sayyidna Ali radhi za Allah ziwe juu yake.
Ama walio dai Mashia kuwa Sayyidna Ali (r.a) ndie anaestahiki ukhalifa na uongozi hakuna dalili juu ya hilo katika Hadithi, kwa sababu hadithi hii Mtume ﷺ alimwambia Ali radhi za Allah ziwe juu yake alipomtaka sayyidna Ali abaki Madina wala asishiriki katika vita Tabuuk na walikuwa Maswaba wote wameshiriki na hakubaki Madina ila wanawake,na watoto na watu wenye nyudhuru. Jambo hio likampa taabu Sayyinda Ali kuona amebakishwa na wanawake na watoto,akamwendea Mtume ﷺ na akamwambia:
أتخلفني في النساء والصبيان
Waniacha na wanawake na watoto, ndio Mtume akamwambia :
[أما ترضى أن تكون مني بمنزلة هارون من موسى]
[Je huridhi uwe kwangu mimi ni kama cheo cha Haruun kwa Musa.]
Na kulikuwa baadhi ya wanaafiq wamesema hangemuacha isipokuwa Hampendi, ndio Mtume akamwambia Sayydna Ali maneno hayo.
[ تاريخ الطبري 3/103-104، والبداية والنهاية لابن كثير 5/7]
[Tarekh- Al-Twabariy 3/103-104 na Al-Bidaaya wa Al-Nnihaya ya Ibnu Kathir 5/7]
2. Na hili la kubakishwa mtu Madina halikuwa ni jambo Hasa kwa Sayyidna Ali radhi za Allah ziwe juu yake, bali kuna Maswahaba kadha Mtume aliwabakisha madina wakati anapo taka kwenda vitani au kwenda Umra au hajji.
Katika vita vya Badru alimbakisha Abdullah ibnu Ummi Maktuum,Radhi za Allah ziwe juu yake
Na katika vita vya Baniy Sulaym,alimuweka Madina Sibaa’I bin Urfatwa Al-Ghifaariy,na katika vita vya Al-Ssawiq alimuweka Bashir Ibnu Al-Mundhir,na katika vita vya Baniy Al-Mustaliq alimuweka Abuu Dhari Al-Ghifariy na katika vita vya Al- Hudaybiyah alimuweka Numayla bin Abdillah Al-Laythiy na wakati wa kwenda kukomboa Makkah alimuweka Kalthum bin Husweyn bin Utba Al-Ghifay,na katika Hijjatul widai (Hijja ya kuaga) alimuweka Abuu Dujaana Al-Ssaidiy
[Tizama sera ya Ibnu Hishaam 2/650,804,806 3/1113-1133-1154]
Kwa hiyo hilo la kubakishwa Ali radhia za Allah ziwe juu yake.
Kubakishwa Madina halikuhusishwa Sayydna Ali peke yake, bali walishirikishwa maswhaba wengine pia, kwa hivyo Mashia hawana hoja katika hadithi kuwa Ali ndie anaestahiki Ukhalifa kwa kudai kuwa Mtume alimuweka Madina awe ni khalifa wake.
Na wanachuoni wamelielezea hilo zamani kuwa Mtume alimwambia sayyidna Ali hilo ili kumridhisha na asihisi vibaya hasa pale wanaafik walipo sema kuwa amemchosha ndio akachukia kufuatana na yeye.
Na kufananishwa kwake na Harun ni pale Musa alipo muacha ndugu yake Harun na yeye kuenda kunon’gona na Mola wake, kisha Mash-huri cha Nabii Musa ,amani ya Mungu iwe juu yao.
3. Na Haruun (a.s) hakuwa khalifa wa Nabii Musa, kwa sabubu Haruni alikufa katika uhai wa Nabii Musa,na Kabla ya kufa Nabii Musa (a.s.) kwa Miaka arubaini kwa hivyo hakuna hoja ya kudai kuwa Sayyidna Ali ndie anaestahiki ukhalifa kwa kufananishwa na Haruun.
Na kule kuambia kuwa wewe ni kama cheo cha Harun kwa Musa ni kwa sababu ya ujamaa wala si kwa lengine.
Kwa hivyo hoja hii wanadai mashia si hoja ya msingi wala hakuna dalili kwa yale wanaodai kuwa Sayyidna ali ndie anaestahiki ukhalifa kwa hadithi hii.
4. Kisha Sayyidna Ali radhi za Allah ziwe juu yake alipa Bay’a Sayyidna Abubakar radhi za Allah ziwe juu yake, na kumkubali awe ndie khalifa wa Waumini baada ya kufa Mtume ﷺ ikiwa Sayyidna ali alifahamu nasi ya hadithi hii, kama walivyo ifahamu Mashia ni kwa nini basi ampe Bay’a Sayyidna Abubakr hali ya kujuwa kuwa yeye ndie anaestahiki ukhalifa ?