الحديث الثالث والثلاثون
“البينة على المدعي واليمين على من أنكر “
عن ابن عَبَّاسٍ رضي اللُه عنهما: أن رسولَ الله صلى الله عليه وسلم قال: [ لَو يُعْطَى النَّاسُ بِدَعْوَاهُمْ لادَّعَى رِجَالٌ أموالَ قَوْمٍ ودِماءَهُمْ لَكِنِ البَيِّنَةُ على المُدَّعِى والْيَمينُ على من أَنْكَرَ]
حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَاهُ الْبَيْهَقِيّ وَغَيْرُهُ هَكَذَا، وَبَعْضُهُ فِي “الصَّحِيحَيْنِ”
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ مُحَمّد بن صَالِح العُثَيْمِين رحمه الله تعالى
HADITHI YA 33
JUKUMU LA USHAHIDI LIKO KWA YULE ANAYEDAI NA KULA KIAPO KUNAMUWAJIBIKIA YULE ANAYEKANA
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas Radhi za Allah ziwe juu yake ambaye amesema kuwa Mtume ﷺ alisema:
[Kama watu wangelipewa kwa mujibu wa madai yao, watu wangelidai mali na damu za wenzao (uhai) lakini jukumu la ushahidi liko kwa yule anayedai na kula kiapo kunawajibika kwa yule anayekana (kuwa hajatenda).]
[Imepokelewa na Al-Bayhaqi na wengineo. Ni Hadithi Hasan.]