باب الرجاء
وعن أَبي هريرة – رضي الله عنه -، قَالَ: كُنَّا قُعُوداً مَعَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -، مَعَنَا أَبُو بَكْرٍ وَعُمْرُ – رضي الله عنهما -، في نَفَرٍ فَقَامَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – مِنْ بَيْنِ أظْهُرِنَا، فَأبْطَأَ عَلَيْنَا فَخَشِينَا أنْ يُقتطَعَ دُونَنَا، فَفَزِعْنَا فَقُمْنَا فَكُنْتُ أوَّلَ مَنْ فَزِعَ فَخَرَجْتُ أبْتَغِي رسولَ الله – صلى الله عليه وسلم -، حَتَّى أتَيْتُ حَائِطاً للأنْصَارِ… وَذَكَرَ الحَدِيثَ بِطُولِهِ إِلَى قوله: فَقَالَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -: {اذهَبْ فَمَن لَقِيتَ وَرَاءَ هَذَا الحَائِطِ يَشْهَدُ أنْ لا إله إلاَّ الله، مُسْتَيقِناً بِهَا قَلبُهُ فَبَشِّرْهُ بِالجَنَّةِ} رواه مسلم
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Tulikuwa tumeketi pamoja na Mtume ﷺ , pamoja nasi alikuwepo Abûbakar na ‘Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake) katika kundi. Mtume ﷺ akaondoka miongoni mwetu, akachelewa kurudi kwetu. Tukahofia asije akawa amedhuriwa. Tukafazaika, tukasimama, mimi nilikuwa wa kwanza kufazaika. Nikatoka kwenda kumtafuta Mtume ﷺ hata nikafika katika bustani moja la Ansari. – akakieleza kisa kwa urefu wake hadi akasema: “Mtume ﷺ akaniambia: [ Nenda, utakayemkuta nyuma ya bustani hili anashuhudia kuwa hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allâh ilihali ya kuyakinisha kabisa neno hili moyoni mwake, mbashirie Pepo.] [ Imepokewa na Muslim ]