0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

387. Riyadhu Swalihina Mlango wa Alama za Allah Kupenda Mja, Mahimizo Kuwa na Tabia Aipendao Allah..

باب علامات حب الله تَعَالَى للعبد والحث عَلَى التخلق بِهَا والسعي في تحصيلها


وعن أَبي هريرة – رضي الله عنه -، عن النَّبيّ – صلى الله عليه وسلم -، قَالَ: {إِذَا أَحَبَّ اللهُ تَعَالَى العَبْدَ، نَادَى جِبْريلَ: إنَّ الله تَعَالَى يُحِبُّ فُلاناً، فَأَحْبِبْهُ، فَيُحِبُّهُ جِبريلُ، فَيُنَادِي في أَهْلِ السَّمَاءِ: إنَّ اللهَ يُحِبُّ فُلاناً، فَأحِبُّوهُ، فَيُحِبُّهُ أهْلُ السَّمَاءِ، ثُمَّ يُوضَعُ لَهُ القَبُولُ في الأرْضِ}    متفق عليه

وفي رواية لمسلم: قال رسول الله – صلى الله عليه وسلم -: {إنَّ الله تعالى إذا أحب عبداً دعا جبريلَ، فقال: إنّي أُحِبُّ فلاناً فأحببهُ، فيحبُّهُ جبريلُ، ثمَّ ينادي في السماءِ، فيقول: إنَّ اللهَ يحبُّ فلاناً فأحبوهُ، فيحبُّهُ أهلُ السماءِ، ثمَّ يوضعُ لهُ القبولُ في الأرضِ، وَإِذَا أبْغَضَ عَبْداً دَعَا جِبْريلَ، فَيَقُولُ: إنّي أُبْغِضُ فُلاناً فَأبْغِضْهُ. فَيُبغِضُهُ جِبريلُ ثُمَّ يُنَادِي في أَهْلِ السَّماءِ: إنَّ الله يُبْغِضُ فُلاناً فَأبْغِضُوهُ، ثُمَّ تُوضَعُ لَهُ البَغْضَاءُ في الأَرْضِ}


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake  amesema: “Mtume amesema: “Allâh Anapompenda mja, Humnadia Jibrîl: ‘Allâh Yuwampenda fulani, nawe mpende.’ Basi Jibrîl humpenda, naye huwanadia watu wa mbinguni (Malaika): ‘Allâh Yuwampenda fulani, nanyi mpendeni,’ nao walioko mbinguni humpenda. Halafu huwekewa kabuli katika ardhi (watu wema wakampenda).”                             [ Wameafikiana Bukhari na Muslim]
Riwaya nyingine ya Muslim imesema: “Mtume amesema: “Allâh Anapompenda mja, Humwita Jibrîl Akamwambia: “Mimi Nampenda fulani nawe mpende. Jibrîl humpenda (mtu yule), kisha hunadi kwa walioko mbinguni akiwaambia: Allâh Anampenda fulani, nanyi mpendeni, walioko mbinguni nao humpenda, kisha (mtu yule) hujaaliwa kabuli katika ardhi. Na (Allâh) Anapomchukia mja, Humwita Jibrîl Akamwambia: Mimi Namchukia fulani nawe mchukie. Jibrîl humchukia, kisha hunadi kwa walioko mbinguni: Allâh Anamchukia fulani nanyi mchukieni. Walioko mbinguni nao humchukia, kisha hujaaliwa uchukivu katika ardhi.
 


Begin typing your search above and press return to search.