BUSTANI YA WATU WEMA
وعن أَبي هُبيْرةَ عائِذِ بن عمْرو المزَنِيِّ وَهُوَ مِنْ أَهْلِ بيْعةِ الرِّضوانِ رضي اللَّه عنه، أَنَّ أَبا سُفْيَانَ أَتَى عَلَى سلْمَانَ وصُهَيْب وبلالٍ في نفَرٍ فقالوا : ما أَخَذَتْ سُيُوفُ اللَّه مِنْ عدُوِّ اللَّه مَأْخَذَهَا ، فقال أَبُو بَكْرٍ رضي اللَّه عنه : أَتَقُولُونَ هَذَا لِشَيْخِ قُريْشٍ وَسيِّدِهِمْ؟ فَأَتَى النَّبِيَّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، فَأَخْبرهُ فقال : يا أَبا بَكْر لَعلَّكَ أَغْضَبتَهُم ؟ لَئِنْ كُنْتَ أَغْضَبْتَهُمْ لَقَدْ أَغْضَبتَ رَبَّكَ ؟ فأَتَاهُمْ فقال : يا إِخْوتَاهُ آغْضَبْتُكُمْ ؟ قالوا : لا ، يغْفِرُ اللَّه لَكَ يا أُخَيَّ . رواه مسلم
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka Abû Hubairah, ‘Â-idh bin ‘Amri al-Muzany naye ni katika watu waliohudhuria Bai‘aturridhwân Radhi za Allah ziwe juu yake amesimulia kuwa Abû Sufyân alimwendea Salmân, Suhaib na Bilâl katika kundi la watu. Wakasema: “Panga za Allâh hazikuwafeka maadui Zake!” Abûbakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) akawaambia: “Mnamwambia hivi mzee wa Maqureshi na Bwana wao?” Akamwendea Mtume ﷺ na akamweleza habari ile. Mtume ﷺ akamwambia: “Eee Abûbakar, pengine umewakasirisha? Iwapo umewakasirisha, hakika umemkasirisha Mola wako.” (Abûbakar) akawaendea na akawauliza: “Enyi ndugu zangu nimewakasirisha?” Wakasema: “Hapana, Allâh Akusamehe ee ndugu yetu.” [Imepokewa na Muslim.]